JAHAZI MODERN TAARAB KUTAMBULISHA NYIMBO ZAO MPYA NDANI YA JIJI LA ARUSHA DECEMBER 11



 
 Mfalme mzee Yusuphy akiwa anawatumbuiza wapenzi wa bendi ya Jahazi modern taarab

Na Woinde Shizza,Arusha



Bendi ya muziki wa taarabu ijulikanayo kwa jina la Jahazi  modern taarab inayomilikiwa na  mfalme mzee yusuphy inatarajia kutua rasmi jijini Arusha kwa ajili ya kuitambulisha  album mpya inajulikana kwa jina la Mahaba niuee.



Akizungumza na waandishi wa habari muandaaji wa onyesho hilo ambaye ni mkurugenzi wa phide entertainment, Phidesia Mwakitalima alisema kuwa  bendi hiii ya jahazi inatarajiwa kutua jijini Arusha na kufanya onyesho lao December 11  ambapo litafanyika ndani ya ukumbi wa Triple A com lex uliopo ndani ya jiji hili.



Alisema kuwa mpaka sasa utaratibu wote umekamilika na wanangoja tu siku ya onyesho ambapo alieleza kuwa onyesho hili litakuwa rasmi kwa ajili ya kutambulisha albamu mpya ya jahazi pamoja na kutambulisha nyimbo zilizopo katika alibamu hiyo.



Aidha alitaja baadhi ya nyimbo zilizopo katika albamu hiyo na ambazo zitatambulishwa kwa wapenzi wa jahazi modern taarabu kuwa ni pamoja na nyimbo iliyobeba albamu  Mahaba niueee,alibainisha kuwa pamoja na uzinduzi huu hii pia itakuwa  ni sehemu ya ziara yao kufunga mwaka Tanzania nzima kwa bendi hii ya muziki wa Taarabu.



Phidesia aliwasihi wakazi wa mji wa Arusha pamoja na vitongoji vyake wajitokeze kwa wingi kwani wasanii wote ,waimbaji wote wacheza show wote na wake wote wa mzee yusuphy watakuwepo katika onyesho hilo.



Aliwataja baadhi ya wadhamini wa onyesho hilo kuwa ni pamoja na Geo security, kwa udhamini mkubwa wa Geo Security Arusha kampuni  bora ya ulinzi, security power fance na alarm  ambapo alisema na katika siku hiyo ya onyesho  watakuwepo pia kwa ajili ya usalama wa wapenzi wote   kuhakikisha mnarudi salama majumbani salama .


Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post