WATAKIWA KUJALI NIDHAMU WAKATI WOTE WA UTUMISHI WAO JESHINI


Askari wapya 1999 waliomaliza mafunzo ya awali Rts Kihangaiko wametakiwa kuhakikisha wanalipa kipaumbele suala la nidhamu wakati wote wa utumishi wao na kuweka mbele kiapo walichoapa kuwa watatekeleza kwa vitendo majukumu yao ya kulitumikia jeshi la wananchi wa Tanzania.

Aidha wametakiwa kuhakikisha kuwa wanakuwa na utayari,Nidhamu,Utii na Uhodari vitakavyowasaidia kuwa wanajeshi wenye nidhamu wakati wote bila kusahau suala la kujiendeleza kielimu kwani ndilo muhimu kwao wakati wote.

Kauli hiyo imetolewa na Mgeni Rasmi Mkuu wa chuo cha mafunzo ya Kijeshi( TMA)Meja jenerali Paulo Massau wakati wakufunga mafunzo ya awali ya RTS Khangaiko kwenye kikosi cha 839 kj wilayani Arumeru huku akisisitiza kuwa suala la kujiendeleza  kielimu linatakiwa kupewa nafasi kubwa kwa wanajeshi hao wapya.

“Mtakapoende kokote hapa nchini mtakapopangiwa suala la Nidhamu ndilo la kwanza kwenu mkiwa kwenye utumishi wenu na nje kwa raia ilikuendeleza sifa nzuri ya jeshi letu la wananchi”aliwaasa Massau.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi kuzungumza na wahitimu hao mkuu wa mafunzo ya awali RTS kihangaiko Luteni kanali Ramadhan Churi aliwaambia mbali na changamoto zilizojitokeza vijana hao wameonyesha kwa vitendo na kuwa anaimani na kuwa askari hodari hapo siku za usoni.

Akwasihi kuzingatia kiapo chao na kuwa mfano kwa utendaji wao wa kazi ili kuipeleka mbali sifa ya jeshi hilo hapa nchini na popote watakapoenda wakati wowote kwenye amani na vita na watambue kukiweka mbele kiapo chao walichaapa.

Kwa upande wake mkuu wa kikosi cha 839kj Luteni Kanali Michael Sijaona Miayala alisisitiza suala la nidhamu na kuwa watajivunia kwao kama watalipa kipaumbele na kuwa maisha yao yote katika utmishi wao suala hilo la nidhamu walipe kipaumbele na ndio nguzo kwa utmishi wao kijeshi na uraini.

Mtambue kuwa maisha yana sehemu mbili katika utumishi wenu kuna utumishi na kustaafu utumishi yote mnatakiwa kuyaandaa sasa bila nidhamu hamtafanikiwa msitumie nafasi zenu katika kuonea raia wala kuonewa nyie bali msingi wenu ni nidhamu katika utumishi mnaoanza leo.

Awali wanajeshi hao wapya 1999 ambao walianza wakiwa 2002 na 8 kuishia kati kwa sababu mbali mbali alionyesha maonyesho mbali mbali ikiwemo kupita mbele ya mgeni rasmi kwa gwaride kwa mwendo wa pole na wa haraka na kutoa heshima hali iliyoleta burudani kwa ndugu na jamaa walioshiriki katika mahafali hayo ya kufunga mafunzo hayo ya awali ya kijeshi.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post