picha ya makamu wa rais Samia Suluhu(picha na maktaba)
Na Woinde Shizza,Arusha
Michuano ya
Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi
Tanzania (SHIMMUTA), yanatarajia kuanza kutimua vumbi wiki ijayo jijini Arusha
kwa kushirikisha Mikoa Yote Tanzania.
Katibu mkuu
wa SHIMMUTA Award Safari alisema kuwa hadi sasa tayari mikoa
kadhaa imethibitisha ushiriki wao ikiwemo wenyeji wa mashindano hayo Mkoa wa
Arusha na Mikoa mingine ni Dar es salaam, Dodoma, Morogoro, Mbeya na Tanga
“Tukiwa kama kamati tendaji ya SHIMMUTA tulifanya kikao tarehe saba mwezi huu
pamoja na wajumbe wa timu shiriki ili kupeana miongozo na taratibu za michezo
hasa tukiwa tunaboresha mapungufu yaliyojitokeza mwaka jana mkoani Tanga”
alisema Safari.
Takribani michezo
12 yatafanyika ikiwa pamoja na Mpira wa Miguu, Riadha, kuvuta Kamba, Mpira wa
Pete, Vishale, karata, na drafti na karata.
“Kwa mujibu
wa katiba, SHIMMUTA ipo chini ya makamu
wa Raisi, hivyo mashindano ya mwaka huu tunatarajia Makamu wa Raisi Samia
Suluhu atakuja kufungua mashindano hayo akiwa anachukua nafasi ya Mlezi
aliyepita makamu wa Raisi Mstaafu Mohamed Ghalib Bilal” Alisema Safari.
Mashindano ya
SHIMMUTA yanatarajia kuanza Novemba 19 hadi Novemba 30 mwaka huu, hivyo timu
shiriki zitaanza kuwasili kuanzia tarehe 17 wakati siku inayofuata SHIMMUTA itafanya
mkutano na viongozi wa timu zote zitakazofika.
SHIMMUTA ni
moja ya mashirika manne yalioundwa na serikali kwa ajili ya kusimamia michezo
makazini ikiwemo SHIMIWI ikiwa chini ya wizara ya kazi, SEMISEMISTA serikali za
mitaa na MAJESHI ambalo linasimamiwa na Baraza la michezo la Majeshi.