ANGALIA MATENGENEZO YA BARABARA YA SANAWARI OLTURUTO -OLDONYOSAPUK
Matengenezo ya barabara ya Sanawari- Olturoto - Oldonyosapuk,
yanaendelea vizuri baada ya kukwama kwa muda, kutokana na zoezi la
kuhamishs mabomba ya maji yaliyokuwa yametandazwa kwenye barabara hiyo.
Mambomba hayo, yanayopeleka maji Jiji la Arusha na kumilikiwa na
Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira AUWSA na kusababisha mradi
huo kushindwa kukamilika kwa wakati na kushindwa kukamilisha mita za
barabara zilizopangwa kutengenezwa kutokana na kiasi cha fedha kutumika
kuhamisha mabomba hayo.
Akizungumza na mwandishi wetu alipotembelea barabara hiyo, Meneja wa
Wakala wa barabara mijini na vijijini 'TARURA', Mhandisi Sangeti Kilusu,
amesema kuwa kwa sasa matengenezo ya barabara hiyo yanaendelea vema,
baada ya kukamilika zoezi la kuhamisha mabomba yaliyokuwa yametandazwa
barabarani.
Kilusu ameongeza kuwa, zoezi la kuhamisha mambomba hayo licha ya
kukwamisha kwa muda shughuli za matengenezo pia limesababisha kushindwa
kutengeneza barabara hiyo kwa muda uliyopangwa, na badala yake
kumalizika mwezi wa Mei badala ya mwezi Machi, 2018.
Aidha mhandisi Kilusu amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa, zoezi la
uhamishaji wa mabomba hayo limeongeza gharama za fedha ambazo
hazikuwepo kwenye mpango ya ujenzi 'BOQ' wakati ukiandaliwa.
"Imelazimika kupunguza ujenzi wa barabara kwa urefu wa mita 300
kutoka mita 1000 zilizopangwa kutengenezwa, na badala yake barabara hiyo
kutengenezwa urefu wa mita 700, kutokana na kulazimika kutumia fedha za
mita 300 kuhamisha mabomba ya maji" amesema Mhandisi Kilusu.
Barabara ya Sanawari-Timbolo inajengwa kwa kiwango cha lami, kwa
urefu wa mita 700 kwa gharama ya shilingi milioni 369 na inategemea
kukamilika mwishoni mwa mwezi Mei, 2018.
About Woinde Shizza
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia