JUMIA FOOD YAFANYA MABORESHO K WENYE PROGRAMU YAKE YA SIMU



JUMIA Food, mtandao unaoongoza kwa huduma ya chakula barani Afrika, umezindua toleo jipya la programu yake ya simu ikiwa na maboresho zaidi yanayotarajiwa kuleta mapinduzi nchini Tanzania. Maboresho hayo yatampatia mteja uwezo wa kipekee wa kuweza kuitumia kwa urahisi zaidi na namna aitakavyo.

“tumejizatiti kuwapatia wateja wetu huduma bora zaidi za kidigitali, huku tukiwahakikishia uharaka wa kufikiwa na huduma ya chakula katika maeneo walipo. Maboresho ya programu yetu ya simu ni mojawapo ya mikakati ya mwaka 2018, pamoja na kuongeza unafuu na urahisi wa upatikanaji wa huduma ya chakula,” alisema Joe Falter, Mkurugenzi Mkuu wa Jumia Food.    

Programu mpya yenye maboresho zaidi, ambayo asilimia 35 ya wateja huitembelea, itaboresha mfumo wa malipo kwa njia ya mtandao pamoja na mawasiliano; ikiwaruhusu wateja kuuliza kuhusu migahawa inayopatikana kwenye Jumia Food kwa mawakala wa huduma kwa wateja. Huduma za chakula zinazofanywa kupitia kompyuta bado zinaongoza kwa asilimia 40, wakati programu ya iOS inayotumiwa na wateja wenye simu za iPhone ikiwa na watumiaji kwa kiwango cha asilimia 25 katika nchi nyinginezo barani Afrika.

Kwa upande wake Meneja Mkazi wa Jumia Food Tanzania, Xavier Gerniers ameongezea kuwa, “maboresho yaliyofanywa kwenye programu mpya ya simu ya Jumia Food hayatoleta muonekano mpya pekee bali pia kuwapatia uwezo wateja kuitumia namna watakavyo hususani kupata taarifa juu ya migahawa waipendayo. Kwa mfano, wateja wanaweza kutafuta aina vyakula wanavyovipenda na kisha programu ikawaletea orodha ya migahawa inayotoa huduma hiyo papo hapo. Tofauti na awali, toleo hili jipya limezingatia urahisi wa wateja kujiunga, kutafuta huduma na kuagiza chakula papo hapo. Cha kuvutia zaidi, wateja wanaweza pia kufuatilia mwenendo wa chakula walichokiagiza kitawafikia ndani ya muda gani!”  

Kwa hivi sasa, programu hii inapatikana kwa watumiaji wa  Android wakati kwa watumiaji wa iOS toleo litatoka mnamo katikati ya mwezi wa Aprili.


“siku zote Jumia Food ipo kuhakikisha inawahudumia watumiaji wa huduma za chakula Tanzania kwa weledi zaidi wakati huo huo ikiendana na mabadiliko ya soko. Tukiwa na zaidi ya migahawa 79 kwenye mtandao wetu, tunaamini kwamba hatimaye tutaweza kuwafikia wateja wote kwa njia ya mtandao,” alihitimisha Bw. Gerniers.  

Kuhusu Jumia Food

Jumia Food Tanzania ni mtandao unaoongoza kwa kutoa huduma ya chakula kwa njia ya mtandao jijini Dar es Salaam. Jumia Food ipo kwenye nchi 11 barani Afrika zikiwemo Kenya, Nigeria, Morocco na Uganda. Huduma hii huwawezesha wateja kwa kupata huduma ndani ya wakati, huongeza wateja, kusaidia uendeshaji na njia za masoko. 

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post