Ticker

6/recent/ticker-posts

UNDP YAISAIDIA TANZANIA MFUMO BORA WA KUKUSANYA NA KUHIFADHI TAARIFA ZA HEWA YA UKAWA

 Na: Calvin Edward Gwabara, Morogoro.


SHIRIKA la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) linaisaidia Tanzania kuwa na mfumo bora wa kukusanya na kuhifadhi taarifa za hewa ya ukaa nchini ili taarifa hizo ziweze kutumika katika mipango mbalimbali ya kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kuwa na taarifa sahihi za mchango wan chi katika kukabiliana na tatizo hilo.
Baadhi ya washiriki mafunzo hayo kutoka wizara mbalimbali na vyuo vikuu wakifuatilia mafunzo ya namna ya kutumia mfumo huo.
Akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa mafunzo kwa wadau wakuu wa mpango huo na namna ya kutumia mfumo huo katika kukusanya taarifa hizo mtaalamu wa miradi inayohusu nishati na mabadiliko ya tabia nchi kutoka UNDP tawi la Tanzania Bwana Abbas Kitogo amesema mfumo huo utaiwezesha Tanzania kuwa na takwimu sahihi za hali ya hewa ya ukaa na namna tunavyopambana katika kuipunguza .
Ameongeza kuwa kwa sasa Tanzania hatuna taarifa sahihi na rasmi sana pale inapotakiwa kueleza mchango wetu kama taifa katika kutatua changamoto hiyo na hivyo kushindwa kujua kama nchi tufanye tuongeze nguvu wapi au tufanye nini katika kusaidia jitihada hizo za dunia.



Aidha amebainisha kuwa kupitia mradi huo wa kujenga uwezo wa serikali katika kujenga mifumo ya jinsi ya kuzia hewa ukaa Tanzania wameamua kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali kama vile wizara na vyuo vikuu lengo likuwa ni kuwawezesha wataalamu wa serikali kuwa na uwezo wa kukusanya taarifa zinazohusiana na mabadiliko ya tabia nchi  na kuzitolea taarifa kule zinakotakiwa.

‘’Tunatakiwa kutoa taarifa kwa umoja wa mataifa ule mpango maalumu wa hewa ukaa na mbadiliko ya tabia ya nchi tunazalisha hewa kiasi gani na mipango yetu ya kupunguza ni kiasi gani na namna ambavyo kama nchi tunaweza kupambana na tatizo hilo hivyo ni muhimu mfumo huu wa taarifa uwepo maana kwa sasa hatuna’’ Alisema Kitogo.


Amesema kuwa Wataalamu wametungenezea mfumo GG inventory System  ambao utakuwa katika hali ya taarifa lakini pia kama tovuti maalumu ambayo itakuwa inasimamiwa ofisi ya makamu raisi lakini watakaokuwa wanaifanyia kazi ni kituo cha kitaifa cha kufuatilia kaboni kilichopo Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo  SUA maana wao ndio wana utaalamu wa kufanya kazi hii.

Ameongeza kuwa kwa kuweka mfumo huo SUA utawezesha wanafunzi pia wanaosoma hapo kuweza kujifunza na kuwa na uwezo kuutumia mfumo lakini pia kuona namna unavyofanya kazi pale ambapo watakutana nao.

‘’Tumepitisha mkataba wa Paris wa kuungamkono juhudi za dunia katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi hasa katika hewa ya ukaa hivyo ni muhimu kuwa na mfumo huo ambao utatuwezesha Tanzania kujitathimini na kuona jitihada zinazofanyika pale tunapotakiwa kutoa taarifa ya nchi kwenye umoja wa mataifa’’ Aliongeza Kitogo.

Amesema kupitia UNDP wameweza kutafuta wataalamu hao na kuwapa kazi ya kutengeneza mfumo huo na baada ya kuutengeneza sasa wameuleta na kuwafonyesha unavyofanya kazi na kuwafundisha namna ya kuutumia maana ni mfumo ambao unabadilika hivyo unahitaji kuboreshwa.


Kwa upande wake mratibu wa kituo cha kitaifa cha kufuatilia hewa ya kaboni kilichopo SUA Prof. Zahabu Eliakimu amesema kuwa mwanzoni wakati walipoanzsha kituo hicho cha kitaifa walikuwa wamejikita kwenye kufuatilia hewa chafu zinazosababisha mabadiliko ya tabia ya nchi walikuwa wanaiangalia zaidi hewa moja ya kabondayoksidi  lakini kupitia mfumo huu watahusisha hewa zote  saba zinazohusika katika kusababisha mabariliki ya tabia nchi.

Amezitaja hewa hizo ambazo mfumo huu utahusika katika kuzifuatilia ukiachia mbali ile ya carbondioxide ya awali ambazo zitaangaliwa katika kila sekta  kuwa ni Green house,Methane,Chlorofluorcarbon,Hydrofluorcarbon,Nitrous Oxide,Walter Vapor pamoja na Ozone.

‘’Tunavyoenda na kuzingalia hewa zote hizi tunabaki kuona kuwa hewa ambayo ndio inaongoza zaidi katika kuchangaia mabadiliko hayo ya tabia ya nchi kuwa ni Carbondioxide lakini hizo nyingine zinachangia kwa kiasi kidogo lakini sekta inayohusika zaidi ni sekta ya matumizi ya ardhi kwenye mistu,kilimo makazi ya watu  ndiyo kupitia madaliko hayo’’ Alisema Prof. Eliakimu.

Kwa upande wake Mataalamu mwandamizi wa mazingira kutoka  ofisi ya makamu wa rais Bi. Adelaida Tillya amesema kuwa mfumo huo ni muhimu sana kwa taifa kwani utaisaidia nchi kuweka mikakati thabiti ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwakuwa sayansi imeonyesha vitu vinavyoweza kuachangia mabadiliko hayo na namna ya kukabiliana nayo kama nchi na mtu mmojammoja.

‘’Tanzania inaonekana haichangii kwa kiasi kikubwa katika mabadiliko ya tabia nchi kama ambavyo zinachangia nchi zingine, lakini ni lazima kuangalia maendeleo ya nchi kama tunapunguza au tunaongeza uzalishaji wa hewa ukaa’’ Alisema Bi. Tillya.

Ameongeza kuwa kwa nchi zinazoendelea zimejiwekea mikakati ya kitaifa katika  kuangalia malengo ambayo nchi imejiwekea kama imefikiwa au la na kuweza kutoa ripoti kwa mamlaka husika kila baada ya miaka miwili kama unavyotutaka Mkataba wa kimataifa  tuliousaini  wa kuungana na nchi zingine duniani katika kupunguza tatizo hili.

Post a Comment

0 Comments