RAIS MAGUFULI KUZINDUA RASMI NYUMBA ZA POLISI ARUSHA APRIL 7



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pohn Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa nyumba za polisi na vituo vya polisi Jijini Arusha.

Akizungumza na waandishi wahabari Kamanda wa polisi jijini hapa DCP Charles Mkumbo amesema kuwa kutakuwa na uzinduzi wa vituo viwili cha Utalii na Diplomasia na kingine ni Kituo cha daraja la kati kilichopo Murieti Jijini Arusha.

Kamanda Mkumbo amesema kuwa kutakuwepo pia na maonyesho mbalimbali ya jinsi Jeshi la Polisi linavyofanya kazi za kuwahudumia wananchi ambapo maonyesho hayo yatafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid .

Amewataka wananchi kutokuwa na hofu kwani hali ya usalama Jijini hapa 
umeimarishwa na amewaomba wajitokeze  kwa wingi katika sherehe hizo.



Kituo cha Polisi cha   Utalii na Diplomasia kinachotarajiwa kuzinduliwa April 7 Jijini Arusha.





Baadhi ya Nyumba za Polisi zinazotarajiwa kuzinduliwa na Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli


About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia