WAKAZI WA KANDA YA ZIWA WAPATA HAMASA YA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA



Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi isiyo ya kiserikali Kivulini Hassan Ally akielezea juu ya mradi wa we can ambao unalenga kuondoa changamoto ya unyanyasaji wa kijinsia .

Mtaalamu wa mitandao ya kijamii kutoka Shirika la Oxfam Bill Marwa akisisitiza akielezea ushiriki wa jamii kwenye mradi wa wanawake tunaweza unaosimamiwa na Taasisi ya Kivulini iliyopo Jijini Mwanza

Mkurungezi wa KONCEPT Krantz Mwantepele akiomba ufafanuzi wa jambo wa maofisa wa kivulini mara baada ya kupata maelezo kuhusu ukatili wa kijinsia katika mikoa ya kanda ya ziwa

Baadhi ya Waandishi wa habari za mtandaoni wakielezewa juu ya Mradi wa Tunaweza katika Taasisi ya Kivulini iliyopo Jijini Mwanza


Taasisi isiyo ya kiserikali ya Kivulini yenye makao makuu jijini mwanza inashughulika na utetezi wa haki za wanawake  kwa kushirikiana na shirika la kimataifa la Oxfam wametoa majumuisho ya mradi wao unaitwa wanawake Tunaweza  mradi ambao  umeanzishwa mahususi kwaajili ya kuhamashisha jamii kushiriki kulinda haki za wanawake dhidi ya ukatili wa kijinsia 

Akizungumzia mradi huo Mkurugenzi mtendaji wa Kivulini Yassin Ally amesema kuwa mradi huo ulianza mwaka 2011  unalenga kuhusisha wanajamii katika kutatua kero zao haswahaswa katika maeneo ya kupinga ukatili wa kijinsia 

Amesema mkoa wa Mara unaongoza kwa asilimia 80% katika  ukatili wa kijinsia  ambao ni kati ya ndoa 10 ndoa 8 zimeshawahi kuwa na viyendo vya ukatili .

Aidha Mkurugenzi ameainisha sababu mbalimbali zinazochangia ukatili wa kijinsia kama 
mila na desturi, Hali duni ya kiuchumi , kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya swala la ukatili  na  mwamko mdogo wa jamii juu ya ukatili wa kijinsia na hii imepelekea katika baadhi ya jamii 
watoto wa kike kuolewa wakiwa wadogo na imechangia kuwaathiri  kifikra kabla ya  kupevuka,

"Wakazi wengi wanategema kilimo kama sehemu ya  kiuchumi na kuinua kipato chao, imebainika kwenye famila nyingi wanaume ndio wamiliki wa nyenzo za uzakishaji kama mashamba nk, hii imechangia sana wakati wa kuvuna wanaume kuwa na sauti juu ya mavuno imeelezwa kuwa wanaume huuza  mazao yote na fedha huzitumia bila kushirikisha wanawake ambao walishugulika kwa pamoja kwenye kilimo  hii imechangia sana kutokea ugomvi ndani ya familia baadhi ya maeneo ya ukanda wa Tarime mwanaume kumpiga mwanamke  kwa kudai fedha za mazao walizouza 

Shirika la Kivulini wametoa mafunzo kwa kwa wanamabadiliko wapatao  150,000 kwa ukanda wa ziwa kwa kuwapa elimu juu ya ukatili ni nini na jinsi ya kuwasaidia wote wanaopata changamoto ya kubaguliwa na kufanyiwa ukatili wa kijinsia pia kundi maalumu  ambalo ni wazee wa kimika ambao wana ushawishi kwenye jamii ili   kuwabadilisha kuhusu juu ya dhana nzima ya ukatili wa kijinsia ,Wakaongea na familia moja moja kwa kuwapa elimu kuhusiana na ukatili wa  kijinsia 

Aidha shirika la kivulini Iimetoa wito juu ya unyanyasaji wakijinsia kuwa upo ,kwa wengine unyanyasaji unaanza ngazi ya kifamilia ,mfano mzazi mmoja kumkashifu mzazi mwenzie mbele ya watoto na kuwaathiri kisaikolojia,

Familia nyingi  zinaaswa zitumie njia ya mazungumzo ili kuifanya jamii iwe na Amani na kujiepusha ukatili wa kijinsia

Changamoto iliyopo katika jamii zetu ni kwamba, watu wanafanyiwa ukatili wa kijinsia majumbani mwao, lakini wanaficha.
Wanakaa kimya badala ya kwenda kuripoti polisi, ili vitendo hivyo visiendelee kutokea.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post