Ticker

6/recent/ticker-posts

Majambazi wenye Silaha za Moto wateka kituo cha Mafuta katikati ya jiji la Arusha na Kupora



Majambazi wapatao wanne wakiwa wamevalia Makoti Meusi na silaha za Moto wamevamia kituo cha Mafuta cha Manjis cha jijini hapa na kufanikiwa kupora kiasi cha sh, milioni mbili zikiwa ni  fedha za Mauzo .


Kwa mujibu wa kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Yusufu Ilembo, akiongea ofisini kwakeleo,tukio hilo limetokea Jana April I6, majira ya saa moja na nusu usiku Katika barabara ya Uhuru katikati ya Jiji la Arusha


Amesema kuwa   majambazi hao walifika eneo la tukio wakitembea Kwa mguu na kuwalazimisha wafanyakazi waliokuwepo katika kituo hicho kulala chini huku wakifyatua risasi mbili hewani na kuelekea ndani ya ofisi zinapohifadhiwa fedha.


Anasema majambazi wawili waliingia ndani huku wawili wakibakia nje kudhibiti raia na baadaye wenzao walitoka wakiwa na  na kiasi hicho cha fedha na kufanikiwa kutokomea kusiko julikana wakiwa wanatembea


Hata hivyo uonyozi wa kituo hicho umelalamikia hatua ya jeshi la Polisi kuchelewa kufika eneo la tukio na hivyo kuwapa nafasi majambazi hao kupora kiulaini na kuondoka bila kubughudhiwa.


Polisi wa doria wanadaiwa kufika baada ya nusu saa zaidi ,ya muda wa tukio na kukuta majambazi wameshatoweka eneo hilo


Kamanda Ilembo amekiri Polisi kuchelewa kufika akijitetea yakuwa Magari ya doria yalikuwa eneo lingine la Kwa Morombo umbali wa takribani kilometa moja toka eneo la tukio na hivyo kuchukua muda kufika .


Katika tukio hilo hakuna ajiyejeruhiwa na Polisi wameanza uchunguzi wa tukio hilo na kwamba hadi sasa hakuna anayeshikiliwa kuhusika na tukio hilo.



Post a Comment

0 Comments