Halmashauri ya Wilaya ya Karatu imefanikiwa kujenga ghala bora la
kisasa kwa wakulima wa vitunguu na ukarabati wa barabara vilivyogharimu
kiasi cha bilioni 3 katika kijiji cha Mang’ora.
Akitoa taarifa hiyo kwa timu ya ukaguzi kutoka taasisi ya Marketing
Infrastricture,Value Addition and Rural Finance Support ( MIVARF) na
Benki ya maendeleo Afrika, Mkurugenzi wa halmashauri bwana Waziri
Mourice amesema halamshauri yake imefanikiwa kutoa 5% katika ujenzi wa
ghala la vitunguu na ukarabati wa barabara.
“Kweli tumejitaidi sana kama halmashauri kutoa 5% ya makusanyo yetu
ya ndani na kufanikisha ujenzi wa ghala na ukarabati wa barabara zenye
urefu wa kilomita 27”.
Ukarabati wa barabara katika bonde la Eyasi umegharimu kiasi cha
bilioni 1.5 na ujenzi wa ghala umegharimu kiasi cha bilioni 1.5 ambapo
na halmashauri ilichangia milioni 153.
Amesema ghala hilo limekuwa msaada mkubwa sana kwa wakulima kwa
kuwaunganisha kwa pamoja kupitia chama chao,pia ghala hilo litawawezesha
wakulima kupanga bei moja ya manunuzi na kuwawezesha kupata masoko ya
ndani na nje ya nchi.
Bwana Waziri ameishukuru MIVARF kwa mchango wao mkubwa katika
kufanikisha shughuli hizo za maendeleo katika halmashauri hiyo na kuomba
zaidi ushirikiano katika kufanikisha shughuli mbalimbali za maendeleo
zikiwemo ujenzi wa kiwanda cha kuchakata mahindi,kufufua kiwanda cha
kusindika maziwa na ujenzi wa hospitali ya wilaya.
Akifafanua zaidia bwana Salum Ramadhani mtaalamu wa mambo ya kilimo
kutoka Benki ya maendeleo Afrika,amesema lengo la timu hiyo kutoka
MIVARF makao makuu ni ukaguzi wa miradi inayofahiriwa na taasisi hiyo
ambao unafanywa kila baada ya miezi 6.
Amesema mradi wa ghala la vitunguu ulilenga zaidi kuweka utaratibu wa
kuwa na soko la pamoja kwa wakulima wenyewe wa vitunguu na hii
itasaidia kupunguza uuzaji wa kiholela kwenda nchi jirani.
Ameipongeza halmashauri kwa kufanikiwa kutoa asilimia 5 ya mapato
yake katika ujezi wa ghala hilo na ukarabati wa barabara kwani ni
halmashauri nyingi zimeshindwa kufanya hivyo.
Aidha, amewashauri wakulima kutafuta masoko ya vitunguu vyao kwa
kutafuta taarifa za bei na masoko kutoka sehemu mbalimbali ili wawe na
uweleza mpana zaidi.
Mwenyekiti wa halmashauri mheshimiwa Jublate Gerson Mnyenye amesema
Changamoto kubwa wanayoipata kama halmashauri ni ujazaji wa maguni kwa
lumbesa inayopelekea wakulima kupata hasara.
Hata hivyo amesema bado wakulima wa vitunguu wanachangamoto ya
mafuriko kuingia kwenye mashamba yao inayopelekea hasara kwa kupata
mavuno hafifu.
Bado halmashauri inaendelea kuandaa utaratibu wa kuwasaidia wakulima
kuweza kusafirisha mazao yao kutoka mashambani hadi kwenye ghala.
Akisisitiza zaidi mratibu wa MIVARF upande wa miundombinu ya masoko
Bwana Jacob Mwambene amesema, wakulima hao wanatakiwa kulitumia hilo
ghala kama malengo yalivyokusudiwa kwa kuwa mradi huo ulilenga kumwinua
mkulima mdogo na wakati katika kilimo cha vitunguu.
Nae katibu wa chama cha wakulima wa vitunguu (LECOFANET) Elia
Bacheng, amesema bado kuna uhaba wa visanduki vya kuwekea vitunguu kwani
vilivyopo havikidhi mahitaji ya sasa.
Aidha,wameiomba serikali iongeze mizani yakupimia magunia yanapokuwa yanaingia katika ghala hilo .
Pia Changamoto nyingine ni kutokuwa na bei maalumu kwa uuzaji wa
vitunguu kwani wanaopanga bei kwa sasa ni madalali ambao baadhi yao ni
wakulima wenzao inayopelekea wakulima kuuza vitunguu vyao kwa hasara.
Ujenzi wa ghala la vitunguu lilifunguliwa rasmi Novemba 2017 kwa
lengo la kuwasaidia uuzaji wa vitunguu kwa wakulima wa vijiji vya
Mang’ola na Baray kuwa na soko moja la pamoja na ujenzi wake
umefadhiliwa na taasisi ya MIVARF kwa kushirikiana na halmshauri ya
wilaya ya Karatu.
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia