picha ikionyesha mtoto Abdul Hussein mwenye Umri wa Miaka 7 mkazi wa daraja Mbili jijini Arusha anayesumbuliwa na maradhi ya Mtindio wa Ubongo pamoja na ulemavu wa viungo anaishi Kwa mateso makubwa kwani tangu azaliwe hajawahi kuamka ,kuona wala kusikia akiwa anapewa maziwa na mama yake Ashura Hussen ,mama huyu anaomba msaada wa kifedha kwa wananchi ,viongozi wa dini ,wabunge pamoja na Rais ili apate fedha za kumpeleka mtoto wake nje ya nchi kwa ajili ya matibabu (picha na Woinde Shizza,Arusha)
baadhi ya waandishi wa habari wakikabidhi vitu ambavyo wamechanga kwa ajili ya kumsaidia mama huyo ambaye ameacha kazi kutokana na kumlea mtoto huyo tangu amzae
Theodora Mrema mwandishi wa Stax Tv akikabidhi sabuni ikiwa ni moja ya michango iliyotolewa na waandishi wa habari wa mkoa wa Arusha
Geofrey Steven mwandishi wa Radio 5 akiwa anakabidi baadhi ya nguo zilizotolewa na waandishi wa habari waliomtembelea mtoto huyo
hawa ni baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Arusha waliojitolea kumtembelea mtoto Abdul anaesumbuliwa na ugonjwa wa mtindio wa ubongo
Na Woinde Shizza,Arusha
Mtoto Abdul Hussein mwenye Umri wa Miaka 7 mkazi wa daraja Mbili jijini Arusha anayesumbuliwa na maradhi ya Mtindio wa Ubongo pamoja na ulemavu wa viongo anaishi Kwa mateso makubwa kwani tangu azaliwe hajawahi kuamka ,kuona wala kusikia.
Mama mzazi wa mtoto Huyo Ashura Hussein Amesema kuwa mtoto wake huyo amekuwa na matatizo tangu azaliwe na aligundulika kuwa na tatizo LA mtindio wa Ubongo akiwa na umri wa miaka miwili
Mtoto wangu Siku nilipojifunga katika hospitali ya Temeke,Dar Siku ya kwanza hakuweza kulia ama kunyonya kama ilivyo kwa watoto wengine.
"Madaktari walimwekea mpira wa maziwa ,baadae baada ya mwaka alianza kunyonya na ilipofika mwaka mmoja na nusu alikuwa akining'ata anapokuwa akinyonya ndipo madaktari wakaniambia ni mwachishe kumnyonyesha ndipo nikamwachisha na akaanza kutumia mpira tangu hapo "Amesema mama Mzazi
Aidha Alisema kuwa alianza kumpa chakula na mpira na alipofikisha umri wa miaka miwili alikumbwa na tatizo kutapika kila anapokula chakula tatizo lililoendelea hadi sasa ambapo kwa sasa anapewa chakula kupitia mrija Kwa kutumia bomba la sindano lakini pindi anapokula akikaa baada ya muda mchache amekuwa akirudisha chakula chote kwa kutapika
"kutokana na matatizo haya kwakweli mimi nilikuwa nesi imenibidi niache sifanyi kazi yoyote nakaa tu hapa nyumbani kwani siwezi hata kwenda kuajiriwa maana siwezi kwenda na mtoto hivyo naishi maisha ya shida sana kusema kweli jamani angalau hata ningekuwa hata na kaofisi ka kuniingizia riziki "aliseama Ashura mama mzazi wa Abudul
Mama Huyo amewaomba wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali wabunge na Rais John Magufuli kuweza kumsaidia ili apate fedha Kwa ajili ya kumpatia matibabu nje ya nchi mtoto huyu .
Hata hivyo wanahabari Jiji LA Arusha wamemtembelea mtoto huyo nakumpatia msaada kidogo wa zaidi ya sh, 300,000 pamoja na mavazi kwa ajili ya mtoto huyo .
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia