Ticker

6/recent/ticker-posts

UHABA WA WAFANYAKAZI WENYE SIFA SEKTA YA UTALII KIKWAZO KATIKA SOKO LA AJIRA NCHINI




Darasa la mafunzo kazini likiendelea  kwa wafanyakazi  wa Hoteli za Chem chem, katika eneo la hifadhi ya jamii ya wanyamapori ya Burunge, wilayani Babati mkoani Manyara

Baadhi ya wafanyakazi wa Hoteli za Chem chem, katika eneo la hifadhi ya jamii ya wanyamapori ya Burunge, wilayani Babat wakipatiwa mafunzo ya lugha ya kiingereza ili kukabiliana na changamoto hiyo

ANDREA NGOBOLE, PMT ARUSHA


Sekta ya Utalii nchini, inakabiliwa na uhaba wa wafanyakazi wenye sifa hatua  inayochangia, kushindwa kupambana na mataifa mengine katika kuvutia watalii hivyo serikali na vyuo vinavyotoa elimu ya Utalii, wameombwa  kuboresha mitaala  ili kwendana na mahitaji katika soko la ajira.

Katibu Mtendaji wa chama cha waajiri katika nchi za Afrika ya Mashariki(EAEO) Dk Aggrey Mlimuka, akizungumzia tatizo la uhaba wa wafanyakazi wa sifa linazikabili nchi zote za afrika ya Mashariki alisema, nusu wa wahitimu wa vyuo vikuu katika nchi hizo, hawana sifa stahiki katika soko la ajira.

Katika kukabiliana na tatizo hilo,Mwekezaji wa Hoteli za Chem chem, katika eneo la hifadhi ya jamii ya wanyamapori ya Burunge, wilayani Babati, ameamua kuanza kuwafunisha wafanyakazi wake 160.

Meneja wa Chemchem Foundation, Charles Sylivesta alisema, wameamua kuwafundisha wafanyakazi,kulingana na mahitaji ya idara zao ili kuwaongezea uwezo wa kufanyakazi hasa kuhudumia watalii.

"wanafundishwa kiingereza,ubishi, kuandaa Vyumba vya kulala watali na kuongoza watalii na tuna wataalam wa ndani na nje ya nchi"alisema.

Meneja wa Chemchem Lodge Kelly  Ricklan alisema mafunzo hayo, yatasaidia wafanyakazi wao ambao wengi wao wanaishi katika eneo la Burunge  kupata uwezo wa kufanyakazi vizuri.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Mwalimu wa lugha  katika hoteli hizo,John Macha alisema, baadhi ya wafanyakazi wamekuwa wakikabiliwa na wakati mgumu kuwasiliana na watalii.

"kipindi hiki hatuna wageni wengi, tumeamua kuwafundisha lugha mbali mbali za kimataifa ili waweze kuwasiliana vyema lakini pia waapewa mafunzo ya wataalam wengine"alisema

Mmoja wa wafanyakazi wa hoteli hizo,Happy Mtani alisema mafunzo hayo, yamekuwa na msaada mkubwa kwao kwani inawasaidia kuoboresha utendaji wa kazi zao

Post a Comment

0 Comments