WATUMISHI WATANO NCAA WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA KUISABABISHIA SERIKALI HASARA YA DOLA ZA KIMAREKANI 35,500
Wafanyakazi watano wa Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro(NCAA])wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kuisababishia hasara serikali na kusababisha hasara ya dola za Kimarekani 35,500.
Ngorongoro(NCAA])wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kuisababishia hasara serikali na kusababisha hasara ya dola za Kimarekani 35,500.
Watuhumiwa
waliofikishwa kizimbani na kukabilia na shitaka moja ni pamoja na
Joseph Mtwala{36},John Mlambo{42},Mwahu Yunus {38},Mery Njau{38} na
Catherini Edward {33}.
Watuhumiwa
hao wote kwa pamoja walisomewa shitaka moja na Mwendesha Mashitaka wa
Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa{TAKUKURU} ,Adamu Kilongozi akiwa
na Hamidu Simbano na Richard Jacopiyo kuwa walitenda kosa hilo kati ya
desemba 25 mwaka 2013 na juni 6 mwaka 2014.
Kilongozi
alidai mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao wakiwa katika lango la Nabi
Mkoani Mara na lango kuu la Loduare Mkoani Arusha watuhumiwa hao
walisababishia serikali hasara ya fedha za Kimarekani kiasi hicho wakiwa
watumishi wa NCAA.
Mwendesha
mashitaka huyo alisoma shitaka hilo mbele ya Hakimu mkazi wa mahakama
ya wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha,Bernad Nganga na kueleza kuwa
walifanya kosa hilo huku wakijua ni kinyume na sheria.
Watuhumiwa
wote walikana shitaka hilo na walipewa dhamana ya fedha taslimu
shilingi milioni 7.9 au mali isiyohamishika yenye thamani hiyo na
taratibu za dhamana zilikuwa zikiendelea .
Mwendesha
mashitaka wa TAKUKURU alisema kuwa ushahidi wa kesi hiyo umekamilika na
aliiomba mahakama hiyo kupanga Tarehe ya kuanza usikilzwaji wa awali
Watuhumiwa wote watano wamepelekwa rumande kwakushindwa kukidhi masharti ya dhamani ,ambapo watasomewa hoja za awali April 10 mwaka huu.

0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia