RAIS MAGUFULI KUZINDUA NYUMBA ZA POLISI JIJINI ARUSHA






Raisi John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Nyumba 18 za Jeshi la Polisi  mkoani hapa zilizojengwa kwa msaada wa wadau mbali mbali wa maenddeleo mkoani Arusha.

Aidha Magufuli atapata fursa ya kushuhudia mazoezi ya utendaji kazi wa jeshi la Polisi katika kujiweka tayari kukubiliana na Uhalifu wa aina yoyote yatakayofanyika katika uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abedi siku hiyo.

Akiongea na waandishi wa Habari Mapema leo,Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo alisema kuwa hafla ya sherehe hizo zitafanyika  April 7 Mwaka huu,ambapo uzinduzi wa Nyumba hizo utafanyika eneo zilipojengwa ndani ya kambi ya jeshi hilo katika makao makuu ya Jeshi la polisi mkoani hapa.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ,Charles Mkumbo


Aidha Raisi Pia atakwenda kuzindua Kituo cha Kisasa cha Polisi Kilichojengwa kwa thamani ya shilingi milioni 265 na Mdau wa  Maendeleo wa jeshi hilo ,Aruna Lodhia kilichopo kata ya Murieti katika jiji la Arusha  Ambacho kitahudumia kwa ukaribu wakazi wa kata hiyo na kata za Jirani.

Kamanda Mkumbo Alisema kuwa Raisi Baada  ya Uzinduzi huo wa nyumba za Polisi pamoja na Kituo cha Polisi Murieti atapata Fursa ya Kushuhudia mazoezi mazito ya kujiweka tayari katika uwanja wa michezo wa Shekh Amri Abedi.

Ambapo mazoezi hayo ni pamoja na Kukimbia na farasi , mazoezi ya Namna mbwa wa Polisi wanavyoweza kuzuia uhalifu na Maandamano.



Mazoezi ya polisi yaliyofanyika mkoani Mbeya


Ujenzi wa nyumba hizo za polisi umetokana na kuungua kwa moto nyumba 13,septemba 27,mwaka jana,na kupelekea familia 13 kukosa makazi ,ambapo raisi Magufuli alichangia shilingi milioni 260 kwa ajili ya ujenzi wa makazi hayo mapya huku wadau na wafanyabiashara mbalimbali jijini hapa wakichangia ujenzi huo.

Kwa sasa jeshi la polisi Mkoani hapa linafanya Mazoezi Mazito ikiwemo kufyatua risasi za Moto na kupiga Mabomu katika uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abedi mbele ya IGP Simoni SIRRO.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia