HII NDIO KAULI YA BALOZI MAIGE KUHUSIANA NA MGOGORO WA ZIWA NYASA


Related image
Kutokana na Taarifa za Raia nane wa Tanzania kukamatwa nchini Malawi kwa kwa kile kinachodaiwa kuwa ni  ujasusi nchini humo  Serikali ya Tanzania Kupitia waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki  Balozi  Dokta Augustino Mahiga amesema juhudi za kumaliza suala hilo linaendelea.
 
Akizungumza jijini  Arusha Waziri Mahiga amesema Serikali ya Tanzania imeshachukua hatua za kumaliza suala hilo ikiwemo kuzungumza na serikali ya ya Malawi.
 
Kuhusu Suala la mgogoro wa Ziwa Nyasa, Balozi Maige ameseama jitihada za kuukwamua  zinaendela chini ya kamati Maalumu iliyoundwa kwaajili ya kutatua suala hilo
 
Watanzania 8 wanaodaiwa kuwa ni majasusi wa Serikali ya Tanzania walikamatwa kamatwa nchini Malawi mwaka jana  kwa tuhuma za kuingia kwenye mgodi wa urani wa Kayerekera uliopo nchini humo kinyume cha sheria.

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.