Ticker

6/recent/ticker-posts

MWIJAGE :TEMDO AKIKISHENI MNAPUNGUZA KASI YA KIWANDA KUFA

Na Woinde Shizza,Arusha
Waziri wa viwanda ,biashara na uwekezaji Charles Mwijage  ameiagiza
taasisi ya uhandisi na usanifu mitambo tanzania (temdo) kupunguza kasi
ya kufa kwa viwanda vingi hapa nchini kwa kuwashauri wajasiriamali na
mashirika makubwa namna ya kuendeleza viwanda wanavyoanzisha kwani
takwimu zinaonyesha viwanda vingi hufa kwa ajili ya ukosefu wa ushauri
wa wataalamu.

Mwijage aliyasema hayo alipokuwa akizungumza katika uzinduzi wa bodi
ya wakurugenzi wa temdo iliyozinduliwa katika ofisi za tasisi hiyo
zilizopo Njiro.

Alisema kuwa viwanda vingi vya wajasiriamali pamoja na makampuni
makubwa hufa kutokana na kukosa ushauri wa wataalamu na hivyo kuitaka
taasisi hiyo ya temdo  kufuata wajasiriamali wanaotegemea kuanzisha
viwanda na kuwapa ushauri ili wajue mbinu na mikakati ya uendelezaji
wa viwanda wanavyoanzisha.

"Viwanda vingi vilianzishwa kipindi cha mwalimu nyerere lakini
inaonekana kuwa asilmia 40 hadi 60 ya viwanda hivyo vimekufa kwa ajili
ya kukosekana kwa ushauri hivyo nielekeze tu kuwa temdo ina haki ya
kuhakikisha inasimamia viwanda ili tanzania iweze kufikia malengo yake
ya uchumi wa viwanda"aliongeza

Alidai kuwa temdo ndio suluhisho pekee la kujenga uchumi wa viwanda
hivyo kutoa rai kwa taasisi na kampuni zinazotaka kuendeleza uchumi wa
viwanda kuhakikisha wanapata utaalamu wa temdo kabla ya kuanzisha
viwanda vyao ili viwanda viweze kuwa endelevu.

Aliongezq kuwa uchumi wa viwanda hauwezi ukajengwa kwa baadhi ya
viwanda kuzalisha bidhaa feki au kiwanda kikiwa chini ya viwango na
kwamba lazima temdo na tbl kusimamia kikamilifu uanzishwaji bora wa
viwanda ambavyo vinakidhi mahitaji.

Awali mkurugenzi mkuu wa temdo mhandisi Kalutu Koshuma alisema kuwa
kwa miaka yote ambayo temdo imekuwepo imeweza kuendeleza teknolojia
nyingi ambazo zimeweza kuchangia uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo
ambavyo vimekuwa mkombozi kwa jamii

Alisema kuwa wamefanikiwa pia kutengeneza kiteketezi cha taka za
hospitalini kwani taka hizo haziruhusiwi kuchanganya na taka nyingine
lakini hata kutengeza mitambo ya kuchomea taka zote ambazo hazifai
kuteketezwa kwa mikono.

Nae mwenyekiti wa bodi iliyozinduliwa  Patriki Makungu alisema kuwa
kama bodi wao watakuwa sehemu ya kutoa ushauri ili temdo iweze kufanya
vizuri zaidi lakini pia watakuwa chachu ya kuifanya temdo iwe endelevu
na hatimae iweze kuwa mkombozi wa uchumi wa viwanda.

Post a Comment

0 Comments