HII TASWIRA YA MAMBO YALIVYONOGA KATIKA UZINDUZI WA WASATU NORTHAMPTON, UINGEREZA

 

Na Freddy Macha 

Jumuiya ya wasanii Watanzania Uingereza (WASATU) ilizunduliwa kwa vigelegele na muziki mjini Northampton , katikati ya Uingereza jumamosi iliyopita. Tafrija hiyo ndogo lakini iliyowakutanisha zaidi ya Watanzania mia moja na marafiki zao wa Kenya, Uganda, Kongo , Nigeria, Uingereza nk, ilihudhuriwa na Mheshimiwa Balozi Dk Asha Rose Migiro. WASATU ilibuniwa mwaka jana kati ya wasanii wakiongozwa na mwanamuziki na mcheza sarakasi Fab Moses na promota wa vyakula vya Kitanzania, Bi Neema Kitilya. Asilimia 20 ya kipato cha onesho zilitolewa na WASATU kwa waliofikwa maafa ya mafuriko ya maji karibuni Tanzania. 1- Watanzania na marafiki zao wakijimwaga Northampton- pic by F Macha 2017 Watanzania na marafiki zao wakijimwaga ukumbi wa The Eastern District Social Club, Northampton.
2-Furaha na shangwe - pic by F Macha 2017Furaha na shangwe ya WASATU 3- Balozi Migiro na Mwana WASATU-mcheza ngoma asilia Khadija Ismail ; wa kwanza ni Salma Kashinde- pic by F Macha 2017Balozi Migiro (katikati) na mwana WASATU- mcheza ngoma asilia, Khadija Ismail. Wa kwanza ni Mtanzania, Salma Kashinde 4-Muziki moto moto Northampton- pic by F Macha 2017Muziki motomoto, Northampton 5-Bango la shughuli 
Bango la shughuli 6-Balozi Migiro akihutubia jumuiko hilo la WASATU- Northampton- pic by F Macha 2017Balozi Migiro akihutubia tafrija 7- Mpiga saxafoni mkongwe na mwana WASATU - Ramasax akipuliza vituz-pic by F Macha 2017Mpiga sasafoni mkongwe na mwanaWASATU- RamaSax- mzawa wa Tanga akipuliza vituz 8- WASATU - 2017WASATU. Toka kushoto nyuma, Rama Sax, Saidi Kanda, John Londo, Fab Moses , Freddy Macha Mbele : Khadija Ismail na Neema Kitilya. Picha na Shah 9- Vitumbua vya Neema KitilyaVitumbua vya Neema Kitilya 10- Nyama ChomaNyama Choma 11- Mwana WASATU -Fab Moses akionesha Sarakasi zakeMwana WASATU Fab Moses akionesha vituko vyake vya Sarakasi 12- Kawele Mutimanwa akikung'uta nyuzi-pic by F Macha 2017Mwanamuziki wa Kikongo aliyehamia Tanzania miaka mingi, Kawele Mutimanwa na bendi ya “Afrika Jambo” jukwaani Northampton 13- Kea toka Kenya aliyesanifu bango la shughuli- pic by F Macha 2017.jpgMwanamuziki mlemavu na msanifu picha, Kea , toka Kenya aliyetengeneza tangazo la WASATU 14-Mboka Lia akitwanga nyuzi zake- pic by F Macha 2017 Mwanamuziki wa Kikongo Mboka Lia ( anayejulikana kwa jina “Burkina Faso”) ndani ya nyuzi na sakata sakata la WASATU
  15-Mwanamuziki mlemavu John Londo- mwana WASATU- pic by F Macha 2017
Mwanamuziki mlemavu aliyekomaa- mtunzi, mwimbaji na mpiga gitaa hatari, John Londo – mwana WASATU aliyebobea. Kileleni Northampton bila kukosa.

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.