BAADHI YA WATUHUMIWA WA UGAIDI ARUSHA WAIGOMEA MAHAKAMA

Kesi ya ugaidi inayowakabili watuhumiwa 61 ikiwemo ya ulipuaji wa mabomu maeneo mbalimbali Jijini Arusha
 Imeendelea kutikisa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Arusha ambako kwa siku ya leo ni watuhumiwa 9 pekee wameweza kufika mahakamani 
Kwa taarifa iliyotolewa na mwakilishi wa uongozi wa magereza mbele ya hakimu mkazi  Gwantwa  Meankuga alidai kati ya watuhumiwa 61 wa kesi za ugaidi ni watuhumiwa  9 pekee walioweza kufika mahakamani siku ya leo
Alisema watuhumiwa hao wameendelea kusisitiza kutofika mahakamani mpaka pale watakapoambiwa upelelezi umekamilika
Pia wakati huo huo wakili wa jamhuri Penina  Johackim aliomba mahakamani  impangie tarehe nyingine kutokana na upelelezi kutokamilika
Hata hivyo,Kaimu Hakimu mkazi Gwantwa Mwankuga alisema kesi hiyo itasikilizwa tena tarehe 25 mwezi aprili

Nimekuwekea majina ya watuhumiwa 9 waliofika mahakamani leo hapo chini.

1. Shaban Idd,
2. Yusuph Ally
3. Sumalya Juma,
4. Kimolo Suleiman
5. Abdallah Juma,
6. Bahan Lazaro
7. Sadick Hussein,
8. Masumau Fadhil
9. Abrahman
Picha 5 kutoka nje ya mahakamani leo  watuhumiwa wakiwasili na kuondoka mahakamani hapo.

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.