SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA JIJI LA ARUSHA
Serikali itaendelea kuboresha huduma za afya kwenye vituo vya afya ,pamoja na Zahanati mbalimbali katika jiji la Arusha.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa mkoa wa arusha Bwana Mrisho Gambo katika muendelezo  wa ziara yake jijini Arusha alipokuwa anazindua nyumba ya mtumishi iliyojengwa na serikali katika zahanati ya NADOSOITO kata yaa Terati jijini hapa.

Nyumba hiyo iliyogarimu kiasi cha shilingi milioni 66.7 ambapo ni mradi unatekelezwa kwa awamu lengo ni kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma za afya katika jiji la Arusha kwa kuwaboreshea makazi watumishi waliopo pembezoni.

Pamoja na hayo faida ya kukamilisha mradi huo umeongeza na kuboresha utoaji  wa huduma za afya katika jiji la Arusha hasa akina mama wajawazito na watoto kutoka kata za Muriet,Terati,Daraja mbili na maeneo jirani.

Mradi huo wa ujenzi wa nyumba ya mtumishi katika zahanati ya NADOSOITO ulianza june 15 mwaka 2016 na utakamilika 15 mwezi wa tano 2017 na mkandarasi anamalizia kwa kuweka marumaru katika nyumba 2 na jiko

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.