Ticker

6/recent/ticker-posts

HOSPITAL ZA SERIKALI ZATAKIWA KUCHUKUA MASHINE ZA KUTEKETEZA TAKA TAKA TEMDO

  • Na Woinde Shizza,Arusha

  • Waziri wa Viwanda Biashara na uwekezaji Charles Muijage ametoa agizo kwa hospitali na zahanati zote nchini kwenda kuchukua mtambo wa kuteketezea taka katika taasisi ya Uhandisi na usanifu mitambo Tanzania[TEMDO] ili kuweza kuteketeza mazalia ya uchafu wa hospitali ili kuweza kutunza mazingira kwani ni taka hatarishi katika mazingira hususani maeneo ya kutolea huduma na maeneo jirani.LAmbapo Taasisi ya Temdo ilianzishwa kwa lengo la kuwa taasisi ya kufanya utafiti kuendeleza na kuhawilisha mitambo ,mashine na vifaa ili kuweza kuwawezesha wawekezaji kubuni na kuunda mitambo,mashine na teknolojia mbalimbali ingawa katika kipindi cha hivi karibuni imekuwa ikikumbwa na changamoto ya uwezeshaji .
  •  
  • Hayo yameelezwa leo na Waziri wa viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Muijage  alipotembelea katika taasisi hiyo na kujionea shughuli wanazoendesha na ambapo katika mambo mbalimbali Muijage anasema kuwa Temdo imekuwa ikibuni vitu mbalimbali ambavyo vinaweza kuwasaidia wananchi na wawekezaji kwa ujumla ingawa wadau wengi wamekuwa hawawatumii ikiwa masuala ya kuteketeza taka katika mahospitali ili kuweza kutunza mazingira.
  •  
  • Waziri Muijage anasema kuwa katika majukumu hayo taasisi ya Temdo inapaswa kwenda kisasa na kwamba kwa kushirikiana na serikali watahakikisha bidhaa zinazoingia nchini zimekidhi viwango na kwamba uchumi wa viwanda utatokana na uwepo wa taasisi h
  •  
  •  Kwa upande wake  Mkurugenzi wa taasisi ya temdo Kalutu Koshuma  ambapo anasema kuwa Temdo inabuni vitu vingi lakini kiteketezi cha taka za hospitali ni muhimu sana kwani mpaka sasa taka hizo zinachomwa kienyeji katika mazingira yaliyopo hapa nchini. 

  • Ameongeza kuwa hivi sasa hospitali na zahanati nyingi zimekuwa zinatumia mtambo wakienyeji hali ambayo inahatarisha hali za wagonjwa waendao kupata huduma katika vituo mbalimbali badala ya kupata huduma za kuponyesgha afya badala yake wanaweza kupata jmadhara mengine ambapoo taasisi hiyo imeamua kutengeneza mtambo huo wakisasa kwajili ya kunusuru mazingira na afya za wakazi wa maeneo jirani.

  • Hata hivyo Mkurugenzi huyo amesema kuwa wanataka kuwezesha taasisi hiyo kuwa wabunifu na kwenda kisasa ili kuwezesha kuendana na teknolojia za kiasasa kwa kadiri nchi inavyihitaji na mahitaji ya soko ya sasa.
  •  
  •  Aliongeza kuwa Ipo haja ya wadau mbalimbali ikiwemo hospitali kujitokeza kutumia ubunifu uliotolewa na taasisi hiyo ili kuweza kuteketeza taka hizo kwa ustadi mkubwa wenye kujali mazingira yanazunguka sanjari na afya za watanzania.

Post a Comment

0 Comments