UJUE MMEA WA GUGU KAROTI UNAOENEA NCHINI KWA KASI TAMBUA NA ATHARI ZAKE
Mwandishi Wa habari kutoka gazeti la The Guardian Edward Qorro akitoa shukrani kwa niaba ya waandishi
Waandishi wakiwa katika Picha ya Pamoja na watoa elimu juu ya gugu Karoti
Kufuatia tishio la mmea hatari unaofahamika kwajina la gugu karoti (Partheniun hysterophorus)kwa afya za binadamu,mifugo na mazingira waandishi wa habari mkoa wa Arusha wamepewa elimu kuhusu mmea huo na kutakiwa kuielimisha jamii kuhusu mmea huo.
Mmea huo wenye madhara kwa binadamu mazao ya mashambani Pamoja na mifugo umesambaa maeneo mengi nchi ikiwemo Arusha ,Kilimanjaro ,Manyara na Kilimanjaro
Asili ya mmea huo umetokea nchini Mexico ,uligundulika miaka ya 1960 ambapo mmea mmoja unauwezo wa kuzaa mbegu 25,000 kwa mche mmoja.
Aidha mmea huo watu wengine wamekua wakiutumia katika shughuli za upambaji , wanatumia kama ufagio, wameyapalilia kama maua majumbani ambapo madhara yake kupata muwasho na vipele mwili nzima.
Mnyama akila majani hayo anaweza kufa maziwa yake yanakuwa machungu yenye uchachu na yanaleta madhara kwa mtumiaji,kwa kuku haiwezi kuendelea kutaga tena.












0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia