Ticker

6/recent/ticker-posts

NANGOLE ASHINDA RUFAA YAKE








Mahakama kuu Kanda ya Arusha imempa siku kumi nne aliyekuwa Mbunge wa Longido Onesmo Ole Nangole kuwasilisha upya notisi ya maombi ya kukata rufaa ya kupinga kuvuliwa ubunge wake alioshinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.


Uamuzi huo umefikiwa hii leo mahakamani hapo chini ya Jaji aliyekuwa akisikiliza shauri hilo Sekela Moshi na kumwagiza mwombaji kuwasilisha maombi hayo huku kila upande ukitakiwa kujigharamia wenyewe.

Jaji Moshi amesema sababu kuu ya kupewa nafasi ya kuongezewa muda kwa muuombaji ni kutokana nay eye kudai palikuwa na ukiukwaji wa haki katika shauri la awali.

Mamombi haya namba 18 ya mwaka 2017 Ole Nangole aliomba kuongezewa muda kuwasilisha notisi upya ya maombi ya rufaa baada ya ile ya mwanzo kuondolewa pamoja na rufaa, maombi  yanayoungwa mkono na hati ya kiapo cha mleta maombi (Ole Nangole) February 23 mwaka huu kwa kuwa na Mapungufu.
Onesmo Ole Nangole kupitia chadema  alivuliwa ubunge wake  Juni 29, mwaka jana na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, kutokana na  kesi ya uchaguzi namba 36 ya Mwaka 2015 iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge kupitia CCM  Dk. Steven  Kiruswa kupinga ubunge huo.

Post a Comment

0 Comments