Ticker

6/recent/ticker-posts

VIONGOZI MSITUMIE HAPA KAZI TU KUWANYANYASA WANANCHI



gambo-1
Mkuu wa mkoa wa Arusha  Mrisho Gambo 

MKUU wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewaonya viongozi wenye tabia ya kutumia kauli ya hapa kazi tu kuwaonea mwananchi.
Akizungumza katika mkutano wa wafanya biashara jijini Arusha uliowajumuisha  TRA na wafanya biashara wa jijini hapa Jana Gambo alisema  baadhi ya viongozi wamekuwa wakitumia vyeo vyao kuwaonea wananchi.
Aidha Gambo alisema  tabia hiyo haitavumulika kwa kuwa serikali ya awamu ya tano imekusudia kuwatetea wanyonge na siyo kuwakandamiza.
"Haiwezekani  watumie vyeo vya uongozi kuwatishia wafanyabiashara pamoja na kuchukua rushwa kwa kutumia kauli ya hapa kazi tu " alisema Gambo.
Alionya tabia ya wafanya kazi wa TRA kuacha kwenda kudai kodi kwa Wateja huku wakiwa wameambatana na askari wenye silaha kuacha tabia hiyo kwani inawatia hofu na kujenga uhasama kati ya TRA na wafanyabiashara.
"Hakuna ulazima wakwenda  kudai kodi mkiwa na askari wenye silaha huku mkiwatishia walipakodi kwa bunduki  wale ni Wateja wenu nendeni kwa utaratibu na endapo mtaona zoezi hilo halifanikiwi ndipo mtachukua  hatua lakini siyo kuwatishia watu" alisema Gambo.
Aliwataka pia wafanya kazi wa TRA  kuwahudumia Wateja kwa ukarimu na waache uzembe kwani Wateja wanapaswa kuhudumiwa vizuri bila kucheleweshwa kwa namna moja au nyingine pindi watakapo Huduma.
Alitumia fursa hiyo pia kuwataka  jeshi  la  polisi kutenda  haki wanapomkamata mhalifu kujiridhisha vya kutosha na siyo kumweka  mtu ndani wakiwa hawana uhakika na kosa alilotenda mtu huyo.
Alisema Mkoa wake hatokubali unafiki wakuletewa majina ya watu akiambiwa ni watumiaji wa madawa ya kulevya  kumbe siyo kweli ni fitina tu.
"Siwezi kukubali kisa mtu anachuki na mtu flani aniletee jina akimtuhumu mwenzake ni mtimiaji  wa  dawa za kulevya  huu utakuwa unafiki  na ninachojua nikiwa mnafiki ujanani ina  maana uzeeni ntakuwa mchawi hivyo siwezi kukubaliana na hilo na badala yake ukiniletea jina nikagundua ni uongo nadili na wewe" alisema.
Naye meneja wa TRA Pili Mbaruku alikiri kuwa watumishi  wa TRA  wamekuwa wakienda kudai kodi huku wakiambatana na watu wa Usalama lakini lengo lao ni kuhakikisha wanaoenda kudai wanakuwa  salama na siyo kwa lengo la  kutishia wateja wao.
"Ni kweli wanaoenda  kudai kodi huambatana na watu wa Usalama ili kuwalinda wawapo  katika kazi hiyo lakini haina maana kuwa kila wanapofika kwa Wateja  nao hushuka kwenye gari hapana wanapaswa kukaa kwenye gari na wasubiri  walioenda kudai kurejea na si vinginevyo" alisema Mbaruku.

Post a Comment

0 Comments