WANANCHI WATAKIWA KULA NYAMA ZILIZOPIMWA NA WATAALAM

Na Woinde Shizza,Arusha

Wananchi wametakiwa kuhakikisha wanakula nyama ambazo zimechinjiwa katika machinjio zinazotambulika kiserikali na zilizopimwa nawataalam wa mifugo ili kuweza kuepuka magonjwa ya milipuko yanayotokana Na nyama.

Hayo yamebainishwa jana na Meneja wa machinjio ya Jiji la Arusha (Arusha Meet)Fabian Kisingi wakati akiongea na waandishi wa Habari ambapo alisema Kumekuwa na magonjwa mengi sana ambayo yanawakumba ng'ombe akiwa ajachinjwa na hata ndani ya nyama baada ya kuchinjwa  iwapo ngombe hatari pimwa na wataalam kunauwezekano mkubwa binadamu akila nyama ile ikamzuru .

Alisema kuwa kumekuwepo na magonjwa ambayo yanapatikana ndani ya nyama  kama vile Kimeta  ,Rifitivale na mengine mengi ambapo pasipo kupimwa na watalaam wa mifugo wanaotambulika Na waliosomea maswala ya mifugo ni ngumu mtu wa kawaida kutambua magonjwa hayo.

"ngoja nitoe  mfano kuna baadhi ya maini yanakutwa Na wadudu na sio rahisi mtu wa kawaida kutambua wadudu hao kwani ni wadogo sana sasa ,watalaam wetu wakipima ndio wanatambua na tukishatambua basis tunachukuwa maini Yale na kwenda kuyateketeza mbali maana maini Yale hayafai kuliwa hata na mbwa" alisema Fabian

Aidha aliwataka wananchi wote wanaochinja ng'ombe zao mitaani kuacha Mara moja maana ni hatari sana kwani huko mitaani akuna mtaalam ambaye anaweza kutambua kama mnyama huyo ni mzima anamaradhi  au sio mzima

"Nichukue fursa hii kuwasihi wananchi kuhakikisha wanachinja mifugo yao mahali panapotambulika kisheria Na palipo na watalaam, sehemu ambayo ukaguzi unafanyika vizuri sehemu ambayo wanaakikisha wanawapa watu nyama nzuri isiyo Na magonjwa Na inayofaa kwa binadamu" alisema Fabian

Kwa upande wake Meneja uzalishaji wa machinjio ya Arusha Meet Happy Ignatius Ngowi alisema kuwa kumekuwepo Na tatizo la wananchi kupeleka ng'ombe zenye mimba kuchinjwa kitu ambacho sio kizuri Na pia ni kibaya kwani kuchwa kule kwa ng'ombe wale kunahatarisha kupoteza uzao mdogo wa ng'ombe.

Alisema kuwa pamoja wananchi wanaona ng'ombe ni wengi lakini kwa wingi huu wa ng'ombe wajawazito wanavyoletwa kuchinjwa kunahatarisha kupoteza uazazi mdogo kwani ng'ombe hawa wengi wanaoonekana kuwepo ambao ni wakubwa kuna ambao wanazeeka na wengine wanakula hivyo iwapo tukiligungia macho hili itafika mahali tutakosa ng'ombe wa kuchinja kabisa

Aliitaka serikali kukemea vikali sana uchinjwaji wa ng'ombe ambao wanamimba Ili kuweza kuendelea kulinda kizazi hichi cha watoto wa dogo .

Meneja WA machinjio ya Arusha Meet Fabian Kisingi akiiongea Na Mwandishi wa habari

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.