Ticker

6/recent/ticker-posts

MANISPAA YA ILALA JIJINI DAR ES SALAAM YAOMBWA KULINUSURU DARAJA ZISISOMBWE NA MAFURIKO


Wakazi wa Gongolamboto wakipita katika  daraja ambalo kingo zake zimesombwa na mafuriko barabara ya kuelekea Machinjio ya Pugu Kajiungeni Dar es Salaam leo.Jitihada za makusudi zisipochukuliwa daraja hilo litasombwa  na maji.
 Mwonekano wa eneo hilo baada ya kusombwa na mafuriko.



Daladala likipita kwenye daraja hilo.

Na Dotto Mwaibale

MANISPAA ya Ilala imeombwa kufanya jitihada za makusudi kuinusuru daraja linaloungani eneo la Gongola mboto na Machinjio ya Pugu ambalo lipokatika hatari ya kusombwa na maji.

Mwito huo umetolewa Dar es Salaam leo na wakazi wa Pugu Machinjioni ambao wamesema iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa mawasiliano kati ya wananchi wa eneo 
hilo na Gongolamboto yatatoweka hivyo kuwa adha kwao kwa kufika makwao kwa kupitia Pugu Kajiungeni badala ya barabara ya Gongo lamboto Pugu Machinjioni kupitia kiwanda cha kutengeneza nguo cha Namera.

"Tunaomba manispaa yetu ilifanyie ukarabati daraja hili ambapo kwa sehemu kubwa kingo zake zimesombwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha " alisema Omari Mshamu mkazi wa eneo hilo.

Mkazi mwingine wa eneo hilo Marietha Stanslaus alisema iwapo daraja hilo linasombwa na maji watakaopata shida zaidi ni wanafunzi kwani watalazimika kutumia njia ndefu kufika mashuleni kwao kutokana kuwa wengi wao wanasoma shule za Gongolamboto.

Jithada za kumpata diwani wa eneo hilo ili kuzungumzia suala hilo zilishindika baada ya kupiga simu yake ambayo haikupatikana.

Post a Comment

0 Comments