Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri akiongea wakati wa
akizugumza na Wakazi wa kijiji cha Mbori,Kata ya Matomondo Wilayani Mpwapwa
wakati wa uzInduzi wa Mnara wa Matomondo. Aidha Airtel pamoja na USCAF
ilizindua minara minne wilayani hapo na kuwawezesha wakazi katika vijjiji 49
kupata huduma za mawasiliano ya uhakika
Meneja wa Kampuni ya Simu ya Airtel,Mkoa wa Dodoma Paschal
Bikomagu akiongea wakati wa akizugumza na Wakazi wa kijiji cha Mbori,Kata ya
Matomondo Wilayani Mpwapwa wakati wa uzInduzi wa Mnara wa Matomondo. Aidha Airtel
pamoja na USCAF ilizindua minara minne wilayani hapo na kuwawezesha wakazi
katika vijjiji 49 kupata huduma za mawasiliano ya uhakika
Mkuu
wa Wilaya ya Mpwapwa,Jabir Shekimweri akisalimiana na mchezaji wa timu ya
Manchester United ya Mbori Wilayani Mpwapwa,Juma Athmani katika mchezo wa
fainali uliochezwa juzi katika uwanja wa Ikulu kata ya Matomondo Wilayani
Mpwapwa. mchezo huo ulikuwa madhumuni kwa ajili ya uzinduzi wa mnara wa simu wa
Matomondo uliojengwa na Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kwa kushirikiana
na USCAF ili kufikisha huduma mawasiliano kwa wananchi waishio maeneo ya
pembezoni mwa nchi. Manchester ilishinda kwa mabao 4-3 dhidi ya Liverpool
Mkuu
wa Wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri akisalimiana na wachezaji wa timu ya Liverpoll ya Mbori Wilayani Mpwapwa
katika mchezo wa fainali uliochezwa juzi katika uwanja wa Ikulu kata ya
Matomondo Wilayani Mpwapwa. mchezo huo
ulikuwa na madhumuni kwa ajili ya uzinduzi wa Mnara wa simu wa Matomondo,uliojengwa
Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na USCAF ili kufikisha
huduma mawasiliano kwa wananchi waishio maeneo ya pembezoni mwa nchi.
Manchester ilishinda kwa mabao 4-3 dhidi ya Liverpool
Airtel washirikiana na UCSAF kufikisha mawalisiano vijiji 49 Dodoma
·
Airtel na UCSAF wazindua minara minne ya mawasiliano mkoani Dodoma
·
Huduma za kifedha kupitia simu za mkononi kuboresha shughuli za kijamii na biashara kwa wakazi wa maeneo hayo
Dodoma, 24
Februari 2017, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel katika
mpango wake wa kufikisha huduma za mawasiliano kwenye maeneo ya
pembezoni imeshirikiana na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa
kujenga na kukamilisha
miundombinu ya mawasiliano katika kata 10 zilizoko katika maeneo ya
vijijini ili kutoa huduma bora ya mawasiliano.
Katika
kufanikisha mkakati huo , Airtel na UCSAF leo imefanya uzinduzi wa
kwanza wa minara minne iliyoko katika kata za Matomondo, Mbuga and Ipera
wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma
ambapo uzinduzi huo utawawezesha wakazi zaidi ya 38,000 katika vijiji
49 kuunganishwa na huduma za mawasiliano toka Airtel na kufurahia huduma
na bidhaa mbalimbali ikiwemo huduma za intaneti, kupiga simu pamoja na
huduma ya Airtel money ili kutatua changamoto
zao
Akiongea
wakati wa uzinduzi wa huduma za mawasiliano katika kata ya Matomondo
Dodoma, Meneja wa mauzo wa Airtel Dodoma, Bwn Pascal Bikomagu alisema”
Airtel imejipanga katika kuboresha
na kupanua upatikanaji wa huduma za mawasilino ili kuchochea kukua kwa
shughuli za kijamii na kiuchumi katika maeneo yaliyo na changamoto
hususani vijijini
“Kufatia
uzinduzi huu leo tunawashauri wakazi wa kata ya Matomondo na vijiji vya
jirani kutumia huduma za Airtel Money katika kufanya miamala ya
kifedha. Huduma hii ya Airtel Money
itawawezesha kutuma na kupokea pesa, kulipia ankra mbalimbali kwa
urahisi na gharama nafuu, na pia kutumiaka kama mfumo rasmi wa huduma
za kifedha kwani upatikanaji wa huduma zingine za kibenki katika maeneo
hayo bado ni changamoto.” Aliongeza Bikomagu
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mh. Jabir Shekimweli Alisema “
mawasiliano ya simu ni nyenzo muhimu katika kukuza uchumi wa jamii na
nchi kwa ujumla, nachukua fursa hii
kuwahimiza wakazi wa kata za Ipera,Matomondo na Mbuga kutumia
mawasiliano hayo katika kuboresha shughuli zao za kilimo na biashara ili
kuinua kipato.
Naye
Mkuu wa Huduma za Ununuzi na Ugavi UCSAF, John Munkondya alisema
“Tunawapongeza Airtel kwakumaliza ujenzi wa minara hii yakutoa
mawasiliano bora, leo hii tumeanza kuzindua
huduma za mawasilino katika mkoa wa Dodoma. ni matumaini yetu
tutaendelea kushirikiana na kuboresha huduma hizi za mawasiliano ili
kuwafika watanzania wengi zaidi.
Airtel ilisaini makubaliano na Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote UCSAF kwa lengo la kufikisha mawasilino katika maeneo ya pembezoni mwa nchi. Kupitia mpango huu kata 28 nchini zimeweza kufikiwa na hivyo kuongeza idadi ya minara ya mawasiliano ya Airtel kufikia 2,210 ndani ya miji zaidi 128 na hivyo kuwafikishia huduma za mawasiliano wakazi zaidi ya asilimia 85 nchin.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia