MAKONDA AWATAJA WAFANYA BIASHARA WA UNGA AWAPA MDA KUJISALIMISHA KITUO CHA POLISI


 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa taarifa ya uchunguzi wake kuhusu biashara ya dawa za kulevya kwenye jiji la Dar es salaam na kuwataja Askari Polisi 9 wanaotuhumiwa kuhusika au kujihusisha na wafanyabiashara wa dawa hizo.

RC Makonda amezitaka mamlaka za kijeshi kuwaweka chini ya ulinzi askari hao kwa mamlaka yake ili waweze kutoa taarifa kwanini dawa za kulevya bado zinaendelea kuwepo.
 
Ameyataja baadhi ya maeneo ambayo Wamiliki wake wamepewa vibali vya kufanya biashara lakini wanatumia maeneo hayo kinyume na masharti ya biashara kwa kuuza dawa ya kulevya ambapo amewataka kufika kituo kikuu cha polisi kesho saa tano na wasipofanya hivyo atawafata mwenyewe.


 'Nimeamua kuingia kwenye hii vita kwa sababu najua Mungu ataniuliza, niko tayari kupoteza ukuu wangu wa mkoa'-RC Makonda

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia