WAZIRI wa Kilimo ,Chakula,Mifugo na Uvuvi Dk.
Charles Tizeba (pichani), anatarajia kufungua kongamano la siku tatu la wadau wa sera za kilimo kesho jijini
Dar es Salaam.
Aidha, kongamano hilo litahudhuriwa na wadau zaidi
ya 200 kutoka nchi mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam jana, Mwenyekiti wa Kampuni ya
Agricultural Non State Actors Forum (ANSAF), Audax Rukonge, alisema serikali
imekusudia kuweka kipaumbele kwenye viwanda vya uchakataji wa mazao ya kilimo.
Kongamano hilo litalenga kuongeza uelewa
miongoni mwa watunga sera kuhusu mchango wa kilimo katika kuhamasisha ukuaji wa
viwanda Tanzani.
“Wadau watajadili kupata tafsiri halisi ya sekta ya
uchakataji mazao ya kilimo katika muktadha wa mageuzi ya viwanda Tanzania,”alisema
Rukonge alisema kongamano hilo limedhaminiwa na
USAID, Benki ya Dunia,ANSAF,JICA na wadau wengine ambao wamesaidia kuleta
watalamu wakiwamo wakulima, watafiti,wafanyabiashara na watunga sera.
Mratibu wa Jukwaa la Sera ya Kilimo na Mchumi
mwandamizi Wizara ya Kilimo, Sophia Mlote alisema kongamano hilo la tatu
litajadili maendeleo ya kilimo nchini ikiwamo kujadili namna ya kutetea
sera,sheria,kanuni.
Pia alisema kongamano hilo litajikita katika
kujadili juu ya mpango wa kilimo cha mihogo,mikunde, samaki, mazao,
usafirishaji pamoja na vifungashio kwa kuwa wazalishaji wengi hawana
vifungashio.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia