BREAKING NEWS

Tuesday, February 14, 2017

MSHIHIRI:MCHEZO WA NDONDI SIYO MCHEZO WA KIHUNI NA NDIO MAANA TUNASAJILI VILABU


Displaying 20170212_182230.jpg
Mwenyekiti wa Ndondi mkoa wa Arusha kwenye meza nyeupe aliyevaa shati la drafti akiwa na Afisa michezo Jiji la Arusha Benson Maneno wakifuatilia mpambano unaoendelea wa ngumi.



Jamii imetakiwa kuondokana na dhana potofu kuwa mchezo wa Ndondi ni mchezo wa kuhuni ,jambo ambalo siyo kweli ni mchezo wa nidhamu unafuata kanuni na taratibu sahihi za mchezo huo bila kukiuka na kuvunja sheria za nchi

Akizungumzia mchezo huo mwenyekiti wa Chama cha Ndondi Mkoa wa Arusha Salim Mshihiri amesema kuwa  mchezo wa Ndondi ni mchezo kama ulivyo michezo mingine ambapo amesema ukipata wafadhili na wachezaji wakiandaliwa katika mazingira mazuri unalilitangaza Taifa na kuliingizia pato taifa pia.

"Mchezo huu siyo wakihuni ndiyo maana tunasajili vilabu kisheria,tukiangalia nchi za wenzetu mchezo huu nathaminiwa sana na wachezaji wa mchezo huu ni matajiri sana,tunaiomba serikali itusaidie kuandaa semina kwaajili ya waalimu wa mchezo huo "alisema Salim.

 Aidha ameiomba serikali kutupia macho mchezo huu,na ameitaka kuusapoti huku akizitaja klab ambazo zipo mkoani hapa zilizosajiliwa ni tano na ya sita amabayo haijasajiliwa Arusha boxing,Katimakutano boxing,Elerai boxing,Kijenge boxing,Sakina boxing pamoja na Long dong ambayo haijasajiliwa.

Kwa upande wake  Afisa michezo Jiji la Arusha Benson Maneno amewataka vijana kujitoa zaidi kushiriki katika michezo mbalimbali ili kujiepusha kujiingiza katika makundi hatarishi ya madawa ya kulevya ambayo yanaharibu nguvu kazi ya Taifa.

Ameutaka uongozi wa chama cha Ndondi katika jiji la Arusha kipindi kingine wakiandaa mashindano ya mchezo huo washirikishe ofisi ya mchezo jiji ili waandae kwa pamoja. 

Sambamba na hayo washiriki wa mchezo huo Meshack Moris ambao walishiriki pambano la ndondi la uzito wa  kg(540 pamoja na Emanuel Juma kg( 54) wamesema kuwa changamoto wanazokabiliana nazo ni pamoja na kukosa kumbi za kufanyia mazowezi,kukosa ulingo.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates