Na Mwandiishi Wetu,kilimanjaro
Katibu mkuu wa CCM Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana leo
ameshiriiki mazishi ya aliyekuwa Katibu wa Hamasa,Sera,Utafiti na
Mawasiliano katika tawi la Shiirikisho la Chuo Kikuu cha Tiba KCMC
marehemu Edwin Christopher Msele aliyefariki katika ajali ya gari huko
Mwika wilayani Rombo Mkoanii hapa.
Kinana ameongoza mamia ya wananchi,wana ccm,wana chuo,wana
familia,ndugu jamaa na marafiki kushiriki mazishi yaliofanyika katika
kijiji cha Kitandu kata ya Okaoni wilaya ya Moshi vijijini mkoani
kiliamnjaro .
Akiwaslisha salamu za Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri
ya Muungwana wa Tanzania Dk John Magufuli ,CCM na jumuiya zake, Kinana
alisema kwa hakika CCM imepokea kwa masikitiko, huzuni na fazaa taarifa
za kifo cha mwanachama huyo.
Alisema marehemu Edwin Msele alikuwa kiongozi wa mstari wa
mbele katika chama kupitia jumuiya ya uvccm na kwamba amepoteza maisha
wakati chama na jumuiya ya vijana ya ccm ikimtegemea na kumuamini.
"Edwin katika uhai wake alitenga muda wake wa kushughulikia
na kujibidiisha n amasomo kwa kujiendeleza kitaaluma pia alikuwa na
matarajio ya kushiriki siasa huku akionyesha uzalendo wa kulitumikia
Taifa lake" Alisema Kinana.
Aidha katibu mkuu huyo wa ccm alisema ccm na Taifa
limempoteza mtu aliyeandaliwa kitaaluma kwa ajili ya kulitumikia Taifa
na watu wake kwani alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa nne akichukua fani ya
utabibu katika chuo kikuu cha kcmc.
"Kwaniaba ya Mwenyekiti wa ccm Dk johnMagufuli,chama cha
mapinduzi na jumuiya zakenawasIkisha salamu za mkono wa pole na
rambirambi kwa wazazi,familia ,ndugu na jamaa kutokanana msiba huo
ulioacha majonzi na huzuni"AlielezaKinana.
Pia Kinana katika msiba huyo amewasilisha mchango wa mkono
wa pole wa ccm na jumuiya zake wakati huku akiwasihi wazazi na familia
ya marehemu Edwin Msele kuwa na mioyo ya subira na ustahamilivu katika
kipindi hiiki kigumu cha msiba na maombolezo.
Hata hivyo katibu mkuub huyo wa ccm alisema vifo vya
wanachama wanne vijana walikuwa na sifa za uchamungu,kupenda elimu na
kwamba walI bar ikiwa kuwa na vipawa na vipaji vilivyohiitaajika katika
jamii.
"Vijana hawa hawatoki katika familia zenye majina makubwa
au familia zenye uwezo mkubwa,ni vijana waliosimama kwa kwa uwezo na
miguu yao ,mishumaa yao ya uhai imezimika,mungu akifunga mlango mmoja
atafungua mingine"Alisema Kinana
Katika mazishi hayo kinana aliambatana na waziri wa
maliasili na utalii Profesa Jumanne Maghembe, Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro
Sadiq Mecky said,Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu
Shaka,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro Idd Juma na Mkuu wa wilaya
ya Moshi Kipi Warioba.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia