TIMU YA WANAHABARI IRINGA YAPIGWA JEKI NA MBUNGE RITTA KABATI

Mbunge  wa  viti  maalum  mkoa
wa  Iringa Ritta Kabati (CCM) akimkabidhi mwenyekiti wa waandishi wa habari mkoani Iringa moja ya jezi alizotoa kwa waandishi wa habari kwa ajili ya mechi mbalimbali za timu hiyo
 Mbunge  wa  viti  maalum  mkoa
wa  Iringa Ritta Kabati (CCM) ameipiga jeki timu ya wandishi wa habari
mkoa wa Iringa kwa kuwapatia   jezi  seti  moja ,mpira na
pesa taslim kiasi cha Tsh  50O,000 ili viwasaidie katika malengo yao
ya kukipiga ligi daraja la kwanza .
na fredy mgunda,Iringa

Mbunge  wa  viti  maalum  mkoa
wa  Iringa Ritta Kabati (CCM) ameipiga jeki timu ya wandishi wa habari
mkoa wa Iringa kwa kuwapatia   jezi  seti  moja ,mpira na
pesa taslim kiasi cha Tsh  50O,000 ili viwasaidie katika malengo yao
ya kukipiga ligi daraja la kwanza .

 Akikabidhi
msaada  huo kwa mwenyekiti wa chama cha wandishi wa habari mkoa wa Iringa
Frank Leonard juzi    mbunge huyo
alisema kuwa  yeye kama mlezi  wa timu hiyo ameamu kujingiza kwa miguu yote
kuisaidi timu hiyo ambayo inaonekana kufanya vema kwenye mchezo wa soka mkoani
hapo .Kabati alisema kuwa licha ya kuwa mpira ni ajira pia
unamsaidia mtu kuwa na afya njema itakayomsaidia kujiepusha na magonjwa yanayoepukika
ikiwemo presha .


“Niwatie moyo hichi mulichokianzisha ni kizuri na timu yenu
ina fanya vizuri na juzi tu mumenyakua kombe la Spanest  kwa kuwanyuka kitisi huu ni ushahidi tosha
mukiendelea hivi hivi mutakuja kuingia ligi daraja la kwanza na baadaye ligi
kuu .

Kabati  aliwataka   wadau  wengine
mkoa  Iringa na nje ya  Iringa  kuendelea  kujitolea
kuisaidia   timu   hiyo    ya
wanahabari ili iendele kufanya vema ndani na nje ya mkoa wa iringaAkipokea vifaa hivyo mwenyekiti wa wanahabari mkoa wa Iringa
Frank Leonard alimshukuru mbunge huyo kwa vifaa na fedha alizotoa huku
akimuahidi mbunge huyo kuwa timu hiyo itakipiga na timu mbalimbali ikiwemo timu
ya bunge la jamuhuri wa muungano wa TanzaniaFrank alisema kuwa timu hiyo imekuwa ikifanya vema kutokana
na kuwa na wandishi wazuri vijana waliona ari ya kusakata kambumbi hivyo ni
vema timu ya bunge kujipanga kisawasa kwani hawata toka salama pindi
watakapokipiga nao mjini dodoma

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.