Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho, akimtunuku Mtihimu wa kwanza wa Falsafa ya Udaktari (PhD), Fadhil Innocent baada ya kuhitimu katika mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB) yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Chuo hicho, Kawe jijini Dar es Salaam. Katikati ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Dk. Costa Mahalu. Kificho alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo.
Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho (katikati), akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Dk. Costa Mahalu (kushoto) na Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho, Jaji mstaafu Steven Bwana baada ya kuwasili kwenye mahafali hayo.
Mtihimu wa kwanza wa Falsafa ya Udaktari (PhD), katika chuo hicho, Fadhil Innocent (wa kwanza kushoto), akiwa na wahitimu wa wengine katika mahafali hayo.
Maandamano yakifanyika kuelekea eneo yalipifanyika
mahafali hayo.
Maandamano yakiendelea.
Wahitimu ndani ya majoho.
Wageni waalikwa wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Wimbo wa taifa ukiimbwa wageni waalikwa wakiwa wamesimama kwa heshima ya wimbo huo.
Mgeni rasmi Mheshimiwa Kificho (katikati), akiwa meza kuu na viongozi wengine. Kutoka kulia ni Mkuu wa Chuo cha Sayansi, Dk.Abdillah Chande, Dean Chuo cha Elimu, Dk.Mary Mosha, Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Dk. Costa Mahalu, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Dk.William Kudoja na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Jaji mstaafu, Steven Bwana.
Wahitimu wa shahada ya kwanza katika ngazi mbalimbali wakiwa kwenye mahafali hayo.
Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Dk.Costa Mahalu akihutubia.
Mgeni rasmi wa mahafali hayo, Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho, akisoma hutuba yake.
Ndugu na jamaa za wahitimu hao wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wageni waalikwa ndani ya mahafali hayo.
Mwonekano katika mahafali hayo.
Mtoto wa Mwanahabari Happyness Katabazi, Queen Japhet Mwaijande, akimpongeza mama yake kwa kutunukiwa shahada ya kwanza ya sheria katika mahafali hayo.
Mtihimu wa kwanza wa Falsafa ya Udaktari (PhD), katika chuo hicho, Fadhil Innocent akiwa katika picha ya pampja na ndugu zake.
Na Dotto Mwaibale
CHUO Kikuu cha Bagamoyo (UB), kimefanikiwa kutoa falsafa ya kwanza ya Udaktari (PHD), licha ya changamoto ya utoaji elimu katika majengo ya kupanga kwa gharama kubwa.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Dk. Costa Mahalu kwenye mahafali ya nne yaliyofanyika leo katika viwanja vya chuo hicho, Kawe jijini Dar es Salaam.
Alisema katika mahafali hayo jumla ya wahitimu 499 wamefanikiwa kumaliza masomo yao kwenye fani mbalimbali, wanafunzi 45 ngazi ya cheti na Stashahada 47.
Wengine waliohitimu shahada 334,Shahada ya udhamiri 71 na shahada ya udamivu ni mmoja licha ya uongozi wa chuo hicho kukutana changamoto nyingi ndani ya miaka mitano lakini wanamshukuru mungu kwa hatua hiyo.
“Namshukuru mungu kwa kutupatia kibali cha kufikia hatua hii ya kufanya mahafali, lakini bado tumekuwa na changamoto ya majengo kwa bado tupo kwenye majengo ya kupanga,” alisema.
Alisema iwapo serikali itabariki kama ambavyo vibali tayari vimetolewa, hivyo watakuwa na uhakika wa mahafali ya mwakani yatafanyika kwenye majengo ya chuo yanayojengwa Kiromo wilayani Bagamoyo.
Aliongeza kuwa chuo kimekuwa na malengo ya kuwasomesha wahitimu wa chuo kwa kuwapeleka vyuo vingine katika shahada ya uzamivu ili kupunguza tatizo la wahadhiri ambalo vyuo vingi nchini wanakabiliana nalo.
Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Amier Kificho aliupongeza uongozi wa chuo hicho kwa jitihada zao za kuendeleza chuo hicho katika mazingira magumu.
Alisema kitendo cha kuendelea kutoa huduma ya elimu inaonesha dhamira ya dhati ya watoa maona kuhusu namna ya kuendeleza elimu nchini Tanzania katika fani mbali mbali.
“Kwa hatua hii hata aliyekuwa anabeza ameanza kujiuliza kuwa tulidhani watashindwa kumbe wameweza, hivyo hiyo itakuwa sifa nzuri ya kusonga mbele,”alisema.
Awali Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Taaluma, Dk.William Kudoja alisema wanaendelea na utaratibu wa kuongeza kozi zingine baada ya kukamilisha ujenzi wa majengo yao Bagamoyo.
“Tunaomba wadau, ikiwamo serikali kuhakikisha wanatusaidia ili kumiliki majengo yetu wenyewe na kuepuka gharama kwenye majengo ya kupanga,” alisema.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia