Ticker

6/recent/ticker-posts

MA MAGUFULI NA MAMA MAJALIWA WATEMBELEA GEREZA LA MAHABUSU LA TABORA, WATOA ZAWADI KWA WAFUNGWA

 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea risala toka kwa Kaimu Mkuu wa
Magereza Mkoa wa Tabora Mkuu wa gereza SSP Nahman Koko wakati yeye na mke
wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walipotembelea Magereza ya mahabusu ya
Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa mahabusu.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkabidhi zawadi  Naibu Mkuu wa
gereza la Mahabusu Tabora Mrakibu wa Magereza Godliver Makwaruzi  wakati
yeye na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walipotembelea Magereza ya
mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu leo
Februari 14, 2017.

Mke wa Rais Mama Janeth magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary
Majaliwa wakiagana na askari magereza bada ya kutembelea Magereza ya
mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu leo
Februari 14, 2017

NA MWANDISHI MAALUM

MKE wa Rais Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary
Majaliwa wametembelea Gereza la Mahabusu Tabora na kutoa zawadi mbalimbali
kwa wafungwa na mahabusu gerezani hapo.

Wake wa viongozi wametembelea gereza hilo leo (Jumanne, Februari 14, 2017)
wakiwa katika ziara  mkoani Tabora, ambapo Mama Janeth amesema wameamua
kuwatembelea wafungwa na mahabusu hao kwa nia ya kuwafariji kwa kuwa wao ni
sehemu ya jamii.

“Vitabu vitakatifu vinasema kwamba ukiwasaidia watu wenye mahitaji utakuwa
umetoa sadaka kubwa kwa Mwenyezi Mungu, hivyo tumeamua kuja kutembelea
 wafungwa na mahabusi kwenye gereza hili na kuwapa zawadi kwa kuwa nanyi
mnahitaji faraja,” amesema.

Amesema wameamua kwenda kuwaona wafungwa na mahabusu hao kwa lengo la
kuwafariji na kuwatia moyo kwa sababu wanaimani kwamba wakitoka watakuwa
raia wema na hayo wanayopitia ni sehemu ya kufanya marekebisho ya tabia.

“Ni siku kubwa kwangu, nimejifunza mengi baada ya kufika hapa. Kitendo cha
kwenda kuwaona wenye mahitaji wakiwemo wagonjwa, wafungwa ni jambo jema
tunaamini hizi zawadi tulizozitoa zitawasaidia kwa sababu tunajua
mnamahitaji mengi,” amesema.

Katika gereza hilo wake hao wa viongozi wamekabidhi zawadi mbalimbali kwa
wafungwa na mahabusu, ambapo mwakilishi wa wafungwa hao Deo Kitave
aliwashukuru kwa niaba ya wenzake. “Tunawashukuru kwa kutukumbuka,
tunamuomba Mwenyezi Mungu muendelee kuwa na moyo huo,”.

Post a Comment

0 Comments