Chama cha Waandishi wa Habari mkoani kilimanjaro (MECKI)
kimesema kimempoteza wanataaluma muhimu aliyekuwa akitegemewa mno na
jamii katika kuitumikia kwa weledi,bidii na ujasiri mkubwa aliokuwa nao
katika maisha yake.
Pia chama hicho kimepokea kwa huzuni na masikitiko makubwa
kifo cha marehemu Anord Swai ambaye pamoja na kufanya kazI za
kitaaluma pia alikuwa mwanachama wa ccm na Mwenyekiti wa uvccm wilaya ya
Hai mkoani hapa.
Mwenyekiti wa media club of kilimanjaro (mecki) Bahati
Mustapha ameiibia uhuru leo nje ya kanisa la kikutheri la usharika wa
Masama mkoani bapa.
Bahati alisema licha ya kwamba marehem alikuwa kiongozi wa
kisiasa pia alimudu kutenganisha ukereketwa wa chama chake na kufuata
maadili ya kitaaluma katika kutimiza majukumu yake ya kihabari katika
jamii.
Alisema mecki imempoteza mwandishi aliyekuwa na ufahamu
,maarifa na upeo mkubwa katika kazi za kihabari kwa dhamira na azma ya
kuitumikia jamiI nyakati zote za maisha na uhai wake.
Aidha alimtaja kama ni mwanataaluma aliyeweza kuukosoa
upande wowotewa kisiasa au serikali kwa kuitumia kalamu yake akiongozwa
na hoja huk mara zote akikataa kuuegemea upande wowote kwa ushabiki wa
kisiasa.
"Tumepokea kwa huzuni na masikitiko makubwa taarifa za kifo
cha Swai,muda mfupi kabla umauiti kumkuta aliweka picha katika ukurasa
wake uso kitabu ya ushiriki wake akiwa katika sherehe za kuzaliwa ccm
huko Rombo"Alisema.
Akimzungumzia marehemu Anord,katibu wa mecki mkoani
kilimanjaro Nakajumo James alisema maisha ya Anord katika tasnia ya
habari yameacha alama pana katika dhati na juhudi ya kuitumikia jamii.
Nakajumo alisema waandishi wa habari wanapaswa kuyaiga
maisha yake kwasababu kila wakati katika kazi ya habari aliweka mbele
kwanza maslahi ya jamii , utaifa na uzalendo kuliko siasa na unazi wake.
"Klabu yetu imepata pengo kwa kuondokewa na mwenzetu
tuliyefanyanaye kazi kwa ushirikiano na upendo,ametuacha wakati bado
jamii,wazazi wake na timu yetu ikimhitaji"Alisema Nakajumo.
Awali mawili wa marehemu Anord ukiwasili nyumbani kwao
katika kijiji cha mweera kata ya Masama,waandishi wa habari waliushusha
na kuuingiza nyumbani kwao baadae kutoa kuelekea katika ushirika wa
kanisa la kikutheri masama kwa ajili ya ibada ya mazishi
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia