Na mwandishi wetu,kilimanjaro
Kanisa katoliki Parokia ya Roho mtakatifu kibosho mango
limewataka madereva wanaoendesha vyombo vya usafri kutambua kuwa
wanabeba binadamu na maisha yao hivyo wanatakiwa kuwa waangalifu na
makini ili kuepuka ajali.
Pia kanisa hilo limehimiza na kuwaasa wanadamu kufanya
ibada ili kujiandaa na maisha baada ya kufa kwasababu uzima wa mikeke
hautapatikana bila kumtumikia mungu
Paroko wa Parokia ya Mango Emma null Tumaini wa kanisa hilo
alitoa maneno hayo ya kiroho leo katika kijiji cha kitandu kata ya
Okaoni huko mosji vijijijni katika adhimisho la misa ya kuiombea maiti
ya marehemu Edwin Msele aliyefariki kwa ajali ya gari huko mwika
wilayani Rombo mwanzoni mwa no ni mwa wiki hii.
Alisema kila dhamana katika jamii inahitaji kutèkelezwa na
binadamu kwa uwajibikaji,ufanisi na umakini mkubwa pamoja na
aliyekabidhiwa dhamana husika akatae kufanya rushwa,manyanyaso maonevu
na kukandamiza haki .
Aidha aliwataka vijana kuvitumia vipaji na karama
walizobarikiwa na mungu kwa minajili ya kujitafutia maisha bora duniani
na kujiandaa kwa uhai mwingine baada ya kifo.
" suala lolote linalowezekana sasa lifanyike mapema kwa
bidii kwasababu wakati ni huu na unapompita binadamu hauna
marejeo,binadamu wafanye kazi za kumpendekeza mungu kwani kazi batili
haijazi thawabu za mja"Alisema Paroko huyo.
Alisema vijana ikiwa watajituma na kutoka jasho halali
wataepukana na maisha duni kwani wakiamua kumtegemea mungu na kuacha
uvuvi na kuzubaa wataishi kwa furaha na upendo.
Aliwaeleza waumini wa dini mbalimbali walioshiriki mazishi
hayo kwamba binadamu anayeishi na kufikisha miaka zaidi ya hamsini na
wengine wakipoteza maisha chini ya miaka hiyo hawana walichompa mungu au
kumkasirisha.
"Mnaohitaji kuuona ufalme wa mbinguni jibidiisheni
kumtumikia mungu kwa kutenda mema,kuwathamini jirani na yatima, kutoa
sadaka kwa kile alichokupa mungu kwasababu mungu hukimbiwi bali
hukimbiliwa"Alieleza paroko Tumaini
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia