WEMA SEPETU AFUNGUKA TENA,AAMUA KUWATOA SHUKRANI,

 Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu leo amefunguka na kuwashukuru mashabiki wake kwa kumpa faraja na kumuombea katika kipindi chote ambacho alikuwa matatizoni.

Kama tunavyo fahamu Wema alitoka kwa dhamana ya shilingi milioni 5 wiki iliyopita baada ya kupandishwa kizimbani kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam ambako alisomewa mashtaka matatu likiwemo la kukutwa na msokoto wa bangi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, wema kaandika.. “Mimi na familia yangu tunapenda kuchukua fursa hii kutoa shukrani zetu za dhati kwa wote mlioshirikiana nasi kwa hali na mali katika kipindi hiki kigumu tulichopitia,”
“Najua wengi mlikua mnaniombea, nashukuru kwa sala na dua zenu kwani zimeni saidia kwa kunipa nguvu wakati nikiwa kwenye wakati mgumu sana kwenye maisha yangu.
Wema aliendelea kutoa shukrani zake kwa wasanii pomoja na mwanasheria wake ambao walikuwa naye katika kipindi hicho kigumu katika maisha yake.

“Napenda kuwashukuru mashabiki wangu wote duniani kwa kuniamini na kusimama na mimi kwa kipindi chote hiki, pia napenda kuwashukuru wasanii wenzangu wote,”
“Asante sana kwa mwanasheria wangu Alberto Msando kwa kunisimamia na kuwa na mimi bega kwa bega wakati huu mgumu.
"Nakuombea kwa Mungu akupe moyo huohuo wa kuwatetea wanyonge. Asante sana. Familia ya marehemu Mzee Issac Sepetu tunasema asanteni sana.” ameongeza.

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.