JESHI LA POLISI ARUSHA LAKAMATA WATU 80 KWA TUHUMA ZA KUFANYA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA

Ishu ya dawa za kulevya imezidi kuchukua headlines kwenye mikoa mbalimbali ambapo leo kutokea Arusha Jeshi la polisi limefanya msako wa dawa za kulevya ambapo leo February 14 2017 limetoa taarifa za matokeo yake.
Kamanda wa polisi Arusha Charles Mkumbo amesema katika msako huo wamekamata mirungi kilo 33, kete 167 za dawa za kulevya aina ya Heroin.
Aidha ameeleza kuwa Jeshi hilo linawashikilia watu 80 akiwemo Askari mwenye namba F. 6978 D/CPL Zakayo ambaye anadaiwa kuchukua dawa za kulevya na kuwabambikiza watu ili aweze kujipatia rushwa.


About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.