Na Mwandishi Wetu,Kiliamnjaro
Kanisa la kilutheri usharika wa Masma limeshauri na
kuzihimiza mamlaka zilizoshika madaraka ya utawala kuwalenga na kuwaibua
vijana wenye upeo,maono na bidii ya kufanya kazi kwa lengo la
kujitegemea.
Pia kanisa hilo limesema vijana ambao hushinda toka
asubuhi hadi usiku wakiwa kwenye,unywaji viroba na uzurururaji
hawataweza kuondokana na kadhia hatari ya ujinga,umasikini na maradhi.
Mchungaji Andrew Munisi aliitoa matamshi hayo leo wakati wa
aibada ya kuiuombea maiti ya marehemu Anord Jonathan Swai ibada
iliofanyika katika usharika wa kanisa la kilutheri la Masama wilayani
Hai mkoani hapa.
Alisema ni jukumu la serikali kuwapatia nyenzo na
uwezeshaji utakaofaa ili vijana walioko hivi sasa katika karakana za
ufundi,viwanda vidogovidogo na ujasiriiamali wapate mwanga zaidi wa
kujituma na kufanyakazi.
Akimzungumzia marehemu Anord,Mchungaji Munisi alimtaja kuwa
ni mfano bora miongoni mwa vijana waliokuwa upeo,maono na maarifa ya
kujituma pia kuitumikia jamii alioishi nayo.
"Tuna kundi kubwa la vijana nchini wenye maono,upeo na
dhati ya kujitoa na kujituma,wanahitaji kusaidiwa na kuwezeshwa ili
wajikwamue, tukiwataza huku wakibaki vilabuni, kunywa viroba na
kuzurura,watapotea "Alisema.
Hata hivyo mchungaji huyo aliwahimiza waumini kuendelea
kumuabudu mungu,kumtegemea na kila mja apime umri wake na jinsi
anavyomtumikia mungu wake.
"Pamoja na Anord kuwa mwanasiasa bado alikataa siasa za
chuki,upasi na mgawanyiko,alitenda mambo kwa wakati huku akimtumikia
mungu wake,chama ,kazi na wazazi wake"Alieleza mchungaji Munisi
Mchungaji huyo wa kanisa la kilutheri alisema kumtumikia
mungu lazima kuambatane na umri wa binadamu katika, maisha yake duniani
kwasababu umri hukimbia mno na mungu atawahukumu wale waliotenda
dhambi.
"Kama tunauhitaji ufalme wa mbinguni hatutaupata mpaka mtu
atamapozaliwa mara ya pili,hata farisayo,tajiri na mjumbe wa baraza kuu
la mayahudi Nicodem alipotaka kujua ufalme wa mbinguni Yesu alimjjbu
amapaka mtu azaliwe mara ya pili"Alisema Mchungaji Munisi.
Anord Swai aliyekuwa Mwenyekiti wa uvccm wilaya ya Hai
mkoani hapa amezikwakwa heshima zote katika kijiji alichozakiwa huko
Mweera kata ya Masama kati wilaya ya Hai mkoani hapa.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia