Na Woinde Shizza,ARUSHA
Bunge la Afrika Mashariki limewapongeza na kuwaenzi hayati spika mstaafu wa bunge la Uganda Jacob Oulanyah na hayati Rais mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki kwa kudumisha demokrasia na utawala bora.
Akichangia hoja hiyo Mbunge wa Afrika Mashariki Fatuma Ndangiza amesema kwamba ipo haja kwa Bunge hilo kuandaa mswada wa kupitisha sheria ya kuwaenzi viongozi waliotangulia mbele za haki ili kuendelea kuwaenzi viongozi na kujenga Utamaduni huo.
Alisema kwamba ukiangalia nchi ya Kenya imekuwa ikisifika kwa katiba bora,hapa utaona mchango mkubwa uliotolewa na hayati Mwai Kibaki kujenga Demokrasia Wakati wa uongozi wake.
Alisema viongozi hao ni wakuigwa mfano Kwa mema yao yote na kuendelezwa na Bunge hilo kuendelea kuwaenzi na kukumbuka mchango wao kwa Taifa lao na mataifa ndani ya Jumuiya.
"Mwai Kibaki alianzisha Katiba na kutoa mchango mkubwa ili nchi iwe na katiba nzuri sasa hivi miongoni mwa katiba ya viwango ni ya Kenya hii inasaidia nchi kuwa na Amani" alisema Ndangiza.
Alisema Bunge hilo linahitajika kuendelea kujenga Utamaduni huo endelevu wa kukumbuka viongozi wetu kwa wabunge kuleta muswada ili uingie kwenye sheria za Jumuiya yetu.
Alisema kwamba Hayati Spika Jacob alisaidia demokrasia ya nchini Rwanda ,alitoa mchango kwa jamii kuwasaidia wenye maisha ya chini na yatima na kuendeleza demokrasia ambayo ikiigwa na vijana itawasaidia
Alisema kwamba jamii zetu katika nchi za Jumuiya yetu zijenge Utamaduni wa kuwaenzi viongozi waliotenda makubwa na kujenga misingi ya ukombozi demokrasia na utawala bora.
Tags
MATUKIO HABARI