Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) komredi Daniel Chongolo, ameendelea kutoa msisitizo kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kushughulikia Tembo Wavamizi wa mazao ya Wananchi mkoani Simiyu.
Ametoa kauli hiyo leo June 02, 2022 wakati alipowasili katika Wilaya Itilima mkoani Simiyu ukiwa ni muendelezo wa ziara yake yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu.