DKT MOLLEL:TOENI HUDUMA BORA KWA WAGONJWA BILA KUSAHAU KANUNI NA MAADILI YA KAZI ZENU

 



Na Woinde Shizza , ARUSHA


Naibu waziri wa afya Dkt Godwin Mollel amewataka watumishi wa afya kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wagonjwa huku wakizingatia kanuni na maadiki ya kazi.



Aidha pia aliwataga wauguzi pamoja na Madaktari kutoa lugha nzuri kwa wagonjwa pamoja na kufata maadili ya uuguzi huku akizitaka taasisi zingine za dini kujenga vituo vingi vya afya ili kuweza kuisadia serikali katika utoaji wa ajira katika sekta ya Afya na wananchi kuendelea kupata huduma bora.



Aliyasema hayo juzi jijini Arusha wakati alipokuwa akifanya ziara yake ya kutembelea hosptali ya Arusha Lutheran medical Center ( ALMC ) ambayo iko chini ya kanisa la KKKT pamoja na hospital ya rufaa ya Mount Meru na pamoja na Chuo cha ukunga na uuguzi kilichopo chini ya hosptali ya ALMC.


Dkt Mollel aliwapongeza watumishi wote wa afya kwa kazi nzuri wanayoifanya huku akiwasihi kuendelea kutoa ushirikiano pindi serikali inapowahitaji katika kutimiza malengo waliyojiwekea ,ambapo alibainisha kuwa katika kipindi cha janga la COVID 19 hospitali ya ALMC ilitoa msaada mkubwa kwa serikali wakati hospital ya mkoa ya Mount Meru ilipozidiwa na wagonjwa katika utoaji wa huduma kwa watalii 


"Nawapongeza watumishi wote wa hospital ya ALMC kwa hatua mliyofikia kutoka bajeti ya dawa ya Shilingi Milion 70 hadi kufika ongezeko la upatikanaji wa dawa kwa bajeti ya milioni 119 na niwaombe mjitahidi ifikapo 2023 bajeti yao ifikie milioni 250,na niwaombe mjitahidi kuboresha hospital hii na watoa huduma hakikisheni mnaondoa migogoro iliyopo na badala yake mfanye kazi kwa weledi na kwa kuzingatia maadili ya kazi pamoja na kuwa na lugha nzuri kwa wagonjwa wenu". Aliongeza Dkt Mollel.



Kwa upande wake Mkurugenzi wa hospital ya Arusha Lutheran medical center ( ALMC ) Elisha Twisa alisema kuwa tatizo la ugonjwa wa uviko 19 imeathiri kwa sehemu kubwa kwa kuwa wagonjwa wengine walishindwa kulipa gharama za matibabu kutokana mitungi ya oxgeni kuwa na gahrama za juu hivyo kusababisha hospital hiyo kuwa na madeni kwa upande wa TRA na NSSF.


Alisema kuwa hospitali hiyo ina malengo makubwa hasa ukizingatia kwa sasa sekta ya utalii imekuwa ,hivyo wanatarajia kujenga hospital kubwa ambayo itaweza kuwahudumia na watalii kwa kuwa utalii ukikuwa na sekta ya afya inaboreshwa zaidi.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post