Ticker

6/recent/ticker-posts

AWESO :AZITAKA BODI ZA WAKURUGENZI WA MAJI KUHAKIKISHA WANAFANYA JUHUDI YA KUZIPATIA JAMII ZA KITANZANIA MAJI MAHALI WANAPOISHI


 



Waziri wa maji Jumaa Aweso  akifungua mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wajumbe wa bodi za mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira  hapa nchini mafunzo yaliyofanyika leo June 29 mkoani Arusha



katibu mkuu wizara ya Maji muhandisi Antoni Sanga akiongea katika mafunzo hayo



Mkurugenzi wa idara ya  usambazaji maji na usafi wa mazingira nchini Joyce Msiru akiongea katika mkutano huo uliofanyika mkoani Arusha Leo June 29 


Na Woinde Shizza ARUSHA


Waziri wa maji Jumaa  Aweso amezitaka bodi za wakurugenzi wa maji hapa nchini kuhakikisha wanafanya juhudi kubwa za kuzipatia jamii za kitanzania maji karibu na mahali wanapoishi ili kuweza ili kuweza kutimiza adhima kuu ya serikali pamoja na kutekeleza ilani ya chama Chama mapinduzi inayosema hadi ifikapo mwaka 2025 huduma ya maji iwe imetolewa kwa asilimia 95 kwa wananchi wa mijini huku vijijini ikiwa imefika kwa asilimia 85. 




Rai hiyo imetolewa leo na waziri wa maji wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya kujengea uwezo wajumbe wa bodi za mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira zipatazo 25 yaliyofanyika jijini hapa ambapo lengo kuu lilikuwa kuwapa ujuzi juu ya usimamizi wa mamlaka zao za maji kama wajumbe wa bodi.



Amesema maji yana umuhimu wa kipekee katika maendeleo ya binadamu kiuchumi na kijamii ambapo upatikanaji wa majisafi, salama na yenye kutosheleza ni nyenzo muhimu katika kuongeza ubora wa maisha, kupunguza makali ya athari zinazotokana na umaskini na kuongeza kipato cha wananchi.



Amesema kuwa mafunzo haya ya siku tatu ni matumaini kuwa yata wajengea uwezo wajumbe hao na kuwataka kuhakikisha wajumbe hao wa bodi wanafanya usimamizi wa pamoja na kuchukua maamuzi makali katika mamlaka hizo.  


“Lengo kuu la kuanzishwa kwa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira ni kuboresha utoaji wa huduma za majisafi na usafi wa mazingira katika maeneo husika” Waziri Aweso amesema.




Naye katibu mkuu wizara ya Maji muhandisi Antoni Sanga amewataka Wajumbe wa bodi kukaa na watumishi wa Idara za maji ili kuweza kuzielewa vizuri na kuweza kuzijua changamoto walizo nazo na kuweza kuzitatua sambamba na kufahamu kazi zinazofanywa na mamlaka zao wanazozisimamia wao na bodi ya Wakurugenzi.




Pamoja na bodi kutakiwa kuchukua hatua stahiki katika uongozi wa mamlaka ikiwemo maswala ya kinidhamu pia zihakikishe zinatatuliwa mapema na kuwambia kuwa sasa hivi wizara ya maji sio ya kulalamikiwa bali ni kutatua changamoto za maji nchini.




Akizungumza kwa niaba ya Wenyeviti wa bodi za maji Mwenyekiti wa Bodi ya maji ya Mamlaka ya maji safi na Maji taka jijini Arusha Dokta Richard Masika amemuhakikishia waziri kuwa kutokana na mafunzo hayo ya siku tatu wana uhakika wa kwenda kuzisimamia mamlaka hizi vizuri na kwa uweledi.



Post a Comment

0 Comments