Mkurugenzi wa Masoko katika Kamisheni ya Utalii Zanzibar Mohamed Mansour wa pili kushoto akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wenzake wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar katika banda lao lililopo katika maonyesho ya karibu Kili fear yanayoendelea mkoani Arusha
Na Woinde Shizza , ARUSHA
Filamu ya Tanzania Royal Tour iliochezwa na Rais Samia imeanza kuonyesha mafanikio mara baada ya wageni kuanza kuingia hapa nchini na kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo hapa nchi
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Masoko katika Kamisheni ya Utalii Zanzibar Mohamed Mansour alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika banda lao lililopo katika maonyesho ya karibu Kili fear 2022 yanayofanyika katika viwanja vya kisongo vilivyopo ndani ya halmashauri ya Jiji la Arusha ambapo alimpongeza Rais Samia Kwa kuandaa filamu hiyo ambayo alisema imesaidia sana kutangaza nchi pamoja na Vivutio vilivyopo
Alisema kuwa tangu kuzinduliwa kwa filamu ya Royal Tour kumekuwepo na ongezeko la watalii kutembelea nchi yetu Kwa ajili ya kuja kuona vivutio mbalimbali vilivyopo ,ambapo pia alibainisha kuwa anaamini jinsi filamu hiyo itavyoendelea kuonyeshwa itawavutia wageni wengi ambao ni watalii na hata wawekezaji kwani katika filamu hiyo Rais Samia ameweza kuonyesha vivutio mbalimbali ,pamoja na fursa ambazo zinapatikana katika nchi yetu.
"Nimpongeze Rais Kwa kitendo alichokifanya Cha ubunifu ambao umeshirikisha pande zote mbili yaani Zanzibar na huku,ameonyesha ninamna gani wanaendelea kuimarisha muungano ,maana hata katika filamu hiyo Rais Samia ameweza hata kumshirikisha Rais wa Zanzibar ili nayeye aweze kuonyesha baadhi ya vivutio vinavyopatikana Zanzibar na kutangaza fursa zilizopo"alibainisha Mohamed
Alisema kuwa filamu hii ni mkombozi kwa nchi yetu kwa sababu kwa muda mrefu tumekuwa tukihangaika kwa kutafuta majukwaa ya kimataifa ya namna gani ya kutangaza vivutio vya utalii.
Alibainisha kuwa filamu hiyo imekuwa mkombozi haswa katika kipindi hichi ambapo mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania zinahaha kujikwamua kiuchumi baada ya janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19.
Akiongelea maonyesho haya alisema wameamua kushiriki ili kuweza kutangaza vivutio mbalimbali vinavyopatikana Zanzibar ikiwemo chumba kilichojegwa ndani ya bahari huko Pemba , shughuli za uvuvi zinazofanywa ,mji mkogwe pamoja na tamaduni mbalimbali zinazopatikana humo
Alisema maonyesho haya ni mazuri na uanasaidia sana kujitangaza kwani watu kutoka nchi mbalimbali wanashiri pia yamesaidia kukutanisha nchi zote za afrika mashariki kwani zikiwemo Kenya ,uganda ,Burundi ,Rwanda na wenyeji Tanzania ambapo alisema nchi ambayo haijashiriki ni Kongo lakini anaamini itashiriki katika maonyesho ya miaka ijayo
Aidha alimalizia Kwa kuwataka watanzania kutembelea vifutio vya utalii vilivyopo hapa nchini kwani masharti yaliyokuwepo awali yamepungua huku alibainisha kuwa wameamua kuungana na Tanzania katika maonyesho haya ili kuunga mkono jitiada za kutangaza filamu ya Tanzania Royal Tour.