Ticker

6/recent/ticker-posts

IGP SIRRO AWAFUKUZA ASKARI POLISI WANAFUNZI ZAIDI YA 100 KWA SABABU MBALIMBALI

 

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema takribani askari polisi wanafunzi 156 wamefukuzwa mafunzo ya Askari Polisi kutokana na sababu mbalimbali.
IGP Sirro amesema hayo leo Juni 29, 2022 wakati alipofanya ziara kwenye uwanja wa medani za kivita wilaya ya Siha, West Kilimanjaro katika Shule ya Polisi Tanzania.

IGP Sirro amezitaja sababu hizo kuwa ni utovu wa nidhamu na kufanya mambo ambayo hayakubaliki ndani ya Shule ya Polisi.
Aidha, amewaelekeza wanafunzi hao wa kozi ya awali ya askari Polisi kufuata sheria, kanuni na taratibu za shule hiyo ikiwa ni pamoja na kudumisha nidhamu ndani ya Jeshi la Polisi

Post a Comment

0 Comments