Na Gift Mongi,Moshi.
Halmashauri ya Moshi mkoani Kilimanjaro imepata hati safi kutoka kwa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG)kwa mwaka wa sita mfululizo jambo linalotajwa kuwa ni matokeo chanya katika usimamizi wa fedha za umma.
Kutokana na hali hiyo ni dhahiri kuwa miradi mbalimbali inayotekelezwa katika halmashauri hiyo ikiwemo hospitali ya wilaya itaenda kutekelezwa na kumalizika kwa wakati kama ilivyo dira ya serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi alisema halmashauri hiyo kupata hati safi inaonesha ni jinsi gani kulivyo na uongozi madhubuti katika usimamizi wa rasilimali fedha na kuwa hiyo inatia moyo kwa serikali kuongeza fedha zaidi za maendeleo.
"Halmashauri yangu ya Moshi nowaponheze wameweza kupata hati safi kwa miaka sita mfululizo sio jambo dogo lakini hozi ni jitihada za mkurugenzi na timu yake na viongozi wengine"alisema
Katika hatua nyingine mbunge huyo aliishukuru serikali kwa kusikiliza kilio
kilio cha wabunge na katika bajeti ya 2022-2023 imeongeza fedha katika bajeti ya kilimo itakayosaidia kupata mbegu bora na pembejeo pamoja na kuongeza mifereji mipya na kuboresha iliyopo tayari kwa umwagiliaji.
Kwa upande wao wadau wa maendeleo Gregory Mmasy alisema halmashauri ya Moshi kuendelea kupata hati safi inatia matumaini sambamba na kuchochea serikali kuendelea kuleta fedha nyingi zaidi.
"Inaonyesha Kuna kazi amabyo inafanyika lakini pia inaonyesha kuna umakini kiasi gani katika usimamizi wa rasilimali maana yake hata tukiomba miradi mingine serikali itatupa kipaumbele"alisema
Brytone Mushi alisema kwa hali ilivyo hivi sasa ni vyema kukawa na usimamizi madhubuti wa rasilimali za nchi kwani ushindani umekuwa mkubwa kwani wanaohitaji maendeleo ni wengi hivyo kukifanyika uzembe kidogo kunaweza kukwamisha maendeleo.
"Yaani viongozi wanaweza kuleta maendeleo au kuyakwamisha ila kwa ilivyofanyika kwa halmashauri yetu ni ni jambo la kuigwa na kuendelea kuwatia moyo ili kuleta maendeleo"alisema