Mkurugenzi wa BOT tawi la Arusha Charles Yamo
Na Woinde Shizza , ARUSHAZaidi ya washiriki mia nne ambao ni wahasibu,wakaguzi na watu wa Benki wanashiriki mkutano wa kujadili taarifa za kifedha zinavyotakiwa kutolewa kwa jamii.
Akizungumza katika mkutano huo mkurugenzi wa bodi ya uhasibu na wakaguzi wa hesabu Tanzania Pius Maneno alisema kuwa washiriki hao wametoka maeneo mbali mbali hapa nchini.
Alisema kuwa dhumuni kuu la katika mkutano huo wataelekezana juu ya huduma za kifedha na utoaji wa taarifa za kifedha za kifedha Tanzania huku mada kumi na moja zikitarajiwa kutolewa.
Aliongeza kuwa mbali na mada hizo pia wataangali visababishi ambavyo vimekuwa vikwazo vya kuwafanya washindwe kufikia malengo ikiwa ni pamoja na kuangalia namna ya kuzuia upotevu kwa kupitia mitandao.
Kwa upande wake naibu gavana wa Benki kuu Charles Yamo alisema kuwa wameamua kukutana kwa pamoja na wataalamu wa fedha ili kuangalia ukuaji wa uchumi.
Aliongeza kuwa moja ya mada ambayo itatolewa kwa washiriki hao ni pamoja na Tehama na kujadili maadili ya utoaji wa huduma nzuri za kifedha kwa wananchi.
Alidai kuwa ili wananchi waweze kunufaika na huduma Bora taasisi za fedha na watoa huduma wanapasawa kuzingatia maadili ili kuwafanya wananchi kuwa karibu nao.