MBUNGE wa Jimbo la Moshi vijijini Prof. Patrick Ndakidemi amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa ya watu na makazi ili kuiwezesha Serikali kupata takwimu sahihi na kuweza kuwahudumia.
Mbunge huyo amesema kuwa lengo la Serikali kufanya sensa ni ili kupata idadi kamili ya wananchi wake na kuweza kuwasogezea karibu huduma muhimu na za msingi kulingana na idadi ya watu.
Alisema kuwa, sensa itaisaidia Serikali kupata taarifa za msingi zitazosaidia katika kuandaa mchakato wa utekelezaji wa dira ya maendeleo kwa mwaka 2025.
"Niwaombe wananchi tutoe ushirikiano wa kutosha siku ya Agosti 23 mwaka huu na tuepuke kutowaficha ndani watoto wenye ulemavu na wazee kwani nao ni haki yao kuhesabiwa ili waweze kupata huduma na mahitaji muhimu kutoka kwa Serikali yao" alisema Prof. Ndakidemi.