Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amemuwakilisha
Waziri wa Maliasili na Utalii katika Mkutano wa Waziri wa Mambo ya Nje
na Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wanaoziwakilisha nchi zao
hapa nchini kuwaelezea mpango wa Serikali katika kulinda na kuhifadhi
eneo la Ngorongoro uliofanyika leo Juni 21,2022 katika Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema kuwa Serikali
imechukua jukumu la kukata eneo la Loliondo SQM 4000 ambazo zina usajili
na eneo la SQM 2500 likakatwa kwa ajili ya matumizi ya Wananchi.
Masanja
amesema kuwa vyombo vya Habari vimekuwa vikipotosha kuhusu eneo hilo
kwa kutaka kuharibu taswira ya wawekezaji nchini Jambo ambalo halina
manufaa kwa Taifa.