![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjuCn1oCOGClq6uZma0XHHomiwbPyZrWHgz9jdqxiMNOwze_GKmPaVwKidiPHNq0_GZcv4HhlOC9-PmPGE3USovjkt_rNe8mmW2uxZ5udSu2__G7gmXhwUbWakqujldjlh7gieRzrqR8RO881Shm-14EHmfdbxPYEaa-sEmj3AOt5NTqtm2XQ/s16000/2.jpeg)
Picha
ya pamoja ya wadau mbalimbali mara baada ya kufunga mafunzo ya
kuangalia afua za kuwasaidia wanaotumia dawa za kufubaza Virusi vya
Ukimwi. Semina hiyo imefanyika kwa siku nne katika Chuo Kikuu Mzumbe
Ndaki ya Dar es Salaam.
JAMII
imeaswa kutowanyoshea vidole watu wanaotumia dawa za kufuvaza Virusi
vya Ukimwi kwani wanasababisha watu hao kutokutumia dawa vile
inavyotakiwa.
Hayo
yamesemwa na Mkuu Mkuu wa Idara ya Masomo ya Biashara kutoka Chuo Kikuu
Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Daktari Omary Swalehe wakati akizungumza
na Mwandishi wetu jijini Dar es Salaam leo, Juni 21, 2022, mara baada
ya kufunga Mafunzo ya siku nne ya wadau mbalimbali.
"Unyanyapaa
imekuwa ni tatizo sugu, imekuwa ni kitu ambacho kinasababisha Wagonjwa
wasitumie Dawa kwa sababu hakuna mtu anapenda aonekane katika jamii kama
anaumwa Ugonjwa au anatumia dawa za Kufubza virusi vya Ukimwi...
Na
kujificha ficha inapelekea watu kutokutumia dozi zao kwa ukamilifu na
kupelekea kuwa na Usugu wa dawa za kufubaza Virusi vya Ukimwi." Amesema
Dkt. Omary
Amesema
kuwa Jamii inatakiwa kuwaangalia watu wenye Virusi vya Ukimwi kama watu
wengine na kuto wanyooshea vidole pindi wanapoenda kuchukua au kutumia
dawa hizo.
Amesema
kuwa Jamii inatakiwa kuelemishwa ili iache kuwanyanyapaa watu wanao
wanaotumia zawa za kufubaza Virusi vya Ukimwi ili waweze kutumia dawa
hizo bila kikwazo chochote.
Amesema
katika matokeo ya utafiti wa awali imeonesha mambo mbalimbali
yanachangia Usugu wa dawa za kufubaza Virusi vya Ukimwi kwa watu
wanaotumia zawa hizo ikiwemwo Umasikini, Umbali wa maeneo ya kuchukulia
dawa kwa wagonjwa pamoja na kutokuwa na fedha za kujikimu wakati
wanapotumia dawa za kufubaza Virusi vya Ukimwi.
Amesema
Matokeo ya Utafiti huo ni utafiti uliofanyika katika wakazi wa Ukonga
na Gongo la Mboto jijini Dar Es Salaam. Aidha ameomba wadau mbalimbali
kuwasaidia wagonjwa hao kwa kuwapa mikopo ili waweze kufanya biashara
ndogo ndogo ili kujipatia kipato kitakacho wasaidia kukidhi mahitaji yao
kipindi chote wanapotumia dawa za Kufubaza Makali ya Virusi vya Ukimwi.
Kwa upande wa serikali wameombwa kupeleka huduma za afya karibu na wananchi ili kuwapunguzia umbali wa kwenda kuchukua dawa.
Mafunzo
hayo yamefadhiriwa na chuo cha KU LEUVEN cha uberigiji wakishirikiana
na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS),
Hospitali za Serikali, Hospitali binafsi na wadau mbalimbali katika
kufanya utafiti juu ya namna ya kukabiliana na Usugu wa Dawa za Kufubaza
virusi vya Ukimwi.
Utafiti
huo umeratibiwa na Prof. Anne-Mieke Vandamme, Prof. Nico Vandaele, Dkt.
Catherine kutoka KU LEUVEN, Prof. Japheth Killewo, Prof. Raphael
Sangeda kutoka MUHAS na Dkt. Omary Swalehe kutoka MUDCC.