Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro Wille Machumu amewataka viongozi wa vyama vya ushirika vilivyolala kutafuta sababu ya vyama hivyo kulala ili kujua namna gani wataaweza kuzipatia ufumbuzi viweze kisimama .
Ameyasema hayo wakati alipokuwa katika mkutano wa jukwaa la maendeleo ya vyama vya ushirika mkoa wa Kilimanjaro Uliofanyika mkoani hapa.
Aidha amesema kuwa kumekuwepo na wimbi la vyama vingi vya ushirika kuanzishwa na kisimama jambo linaloonesha kutoleta maendeleo kwa vyama hivyo.
"Nitoe Rai vile vile hivi vyama ambavyo vimesinzia tutafute tu sababu ya usinziaji wa vyama hivyo, maanake tukaeza kuendelea kuhamasisha ,tunaanzisha ,vinapungua kwa hiyo basi tuangalie ni Nini chanzo kwani inawezekana ni uongozi" Alisema Machum.
Amesema ni vyema kuangalia ni namna gani ya kuweza kuangalia ni namna gani ya kuweza kuanzissha viwanda vya kuyachaakata maazao wanayozalisha.
"Ushirika Sehemu Nyingi ndio umejenga makampuni na yakaanzisha na viwanda kwa hiyo naomba tujenge ushirika ambao ni mzito,na tufike mahali ya kuongeza thamani kwenye mazao badala ya kuyauza Kama yalivyo."Alisema Machum.
Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika Jaclin Senziga ameeleza Hali ya vyama vya ushirika Mkoa wa Kilimanjaro na faida zinazotokana na vyama hivyo ambapo amesema Kuna mafanikio yaliyopatika kutokana na vyama hivyo vya ushirika ambayo ni pamoja na halmashauri kupata mapato kutoka kwenye kwenye mauzo mbalimbali ya mazao .
Kwa upande wake mwenyekiti wa jukwaa la vyama vya ushirika mkoa wa Kilimanjaro Bosko Simba ameishukuru Serikali kwa kuonesha ushirikiano na kisimamia shughili zote za kiushirika nchini.
Amesema kuwa watatoa ushirikiano kwa Serikali na Wizara ya kilimo ili kuwezesha kufika na kuvuka malengo ya mkoa na Taifa Kwenye Ujenzi wa Usharika na Sekta nyingine.
"Tunatarajia kuuendeleza na kuonesha tofauti na mikoa mingine hasa katika ubora unaotakiwa na ufanisi unaostahili kwani tumejaliwa kuwa na chuo Cha ushirika katika mkoa wetu hivyo hatuna budi kuwa mfano wa kuigwa.Alisema Simba.
Washiriki walioshiriki katika kongamano Hilo wameeleza ni namna gani itawasaidia Kama viongozi na kuwakumbusha wajibu wa kazi zao.